Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi akizungumza jana na walegwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF) katika Kijiji cha Kinamagi wilayani Uyui Mkoani Tabora
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF) katika Kijiji cha Kinamagi wilayani Uyui Mkoani Tabora Enviolatha Kamage (aliyekaa mbele ya cherehani) akimuonyesha jana Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi(kushoto) jinsi alivyoweza kunufaika na fedha hizo hadi akanunua cherehani na kujenga nyumba.
Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi(wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Eviolatha Kamage( wa saba kutoka kushoto) na viongozi wengine katika ziara yake jana kwenye kijiji cha Kinamagi wilayani Uyui mkoani Tabora.
Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi(kulia) akiangalia jana mbuzi wa mmoja wa wanufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji cha Kinamagi wilayani Uyui mkoani Tabora.
…………………………………………………………………………….
Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amewasa walegwa wa Mpango wa Kusuru Kaya Masikini (TASAF) kuacha kuzitumia fedha wanazopatiwa kwa matumizi ya starehe na anasa.
Alisema kwamba fedha wanazopatiwa wanapaswa kuzitumia kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kusonga mbele ili maisha yao yawe tofati na wakati ambapo walikuwa hajaanza kupata fedha hizo.
Alisema kwamba kila mlengwa anatakiwa kutumia fedha hizo vizuri kwa ajili ya kuisaidia familia kwa kuwapeleka watoto shule,klinick na kujiwekea akiba .
Aidha aliwataka maafisa ugani kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda kutoa elimu kwa walegwa na Tasaf ili kuweza kufanya ufagaji ulio bora.
Awali Katibu Tawala Msaidizi(Mipango na Uratibu ) mkoani Tabora Rukia Manduta alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa toka mwaka 2015 hadi 2020 jumla ya shilingi bilioni 39.9 zimetolewa kwa walengwa.
Alisema kiasi hicho cha fedha kimewawezesha lipata elimu ya Ujasiriamali inayotolewa na wataalamu katika kila dirisha la uhaulishaji, lengo ni kuwasaidia kaya hizo kuibua miradi midogo itakayo wawezesha kuongeza kipato.
Manduta alisema hatua inesaidia Kaya za walengwa kupata uhakika wa chakula cha kuwafanya wapate mlo mara tatu
Manduta aliongeza kuwa sanjari na hayo jumla ya walengwa 26,193 wamejiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF).
Alisema kuwa kaya za walengwa zilizopo kwenye mpango zimeweza kuanzisha miradi midogo midogo kama vile Mama Lishe, kilimo cha bustani, ufugaji wa Kuku, Mbuzi, Ng’ombe, Nguruwe, Kondoo pamoja na Ufugaji wa Nyuki.