Home Biashara WAZIRI MKENDA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI CHA PYXUS DODOMA,AWATOA...

WAZIRI MKENDA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI CHA PYXUS DODOMA,AWATOA HOFU WAWEKEZAJI WA MAZAO YA MAFUTA

0

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akitoa maelekezo kwa viongozi wa wizara hiyo na viongozi wa kiwanda cha Pyxus alipokitembelea leo Januari 22,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akipatiwa maelezo ya uzalishaji wa mafuta katika kiwanda cha Pyxus kilichopo jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukitembelea leo Januari 21,2021.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akikagua uzalishaji wa mafuta katika kiwanda cha Pyxus kilichopo jijini Dodoma alipokitembelea leo Januari 22,2021.

……………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali imesema imewekeza nguvu kubwa katika kuzalishaji wa mazao ya mafuta ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza mara kwa mara za uhaba wa mafuta hapa nchini ili kupunguza uagizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa leo Januari 22,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Prof. Adof Mkenda alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha PYXUS kilichopo Kizota jijini Dodoma, amesema umefika wakati sasa wa wakulima kuandaa mashamba kwa kufuata ushauri wa utaalamu ili kupata mazao mengi.

“Sisi kama serikali tunajipanga kuhakikisha kunakuwa na mbegu za kutosha,tunaweka nguvu kubwa kwenye uzalishaji wa mazao ya mafuta,ukiangalia sasa hivi tunatumia takribani nusu trilioni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje,sisi kwenye mfumo rasmi  tunazalisha asilimia 47 tu” amesema Prof Mkenda.

Aidha Profesa Mkenda amewataka wakulima kutumia fursa ya uhaba wa mafuta iliyopo kwa kuongeza uzalishaji wa  mazao ya mafuta na kutumia changamoto hiyo kama fursa ya kujiongezea kipato,kuongezea nchi kujitegemea kwenye mafuta ya kula na kupata fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa hizo nje ya nchi.

Amekemea tabia ya urasimu lililopo bandarini katika utoaji wa vibali vya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na kusema yoyote mwenye tabia hiyo hatakuwa na nafasi katika utawala huu.

Amesema ni utaratibu mbovu kwani haiwezekani kama nchi kukwamishwa na mtu mmoja wakati tunahitaji wawekezaji wengi hapa nchini kuongeza vipato kwa wananchi na kuongeza bidhaa.

Ameongeza kuwa “kuna makontena yapo bandarini kuna maafisa wamekalia tu hawataki kutoa vibali,natoa wito kwa maafisa hao wajue kwenye uchumi tunaoenda lazima twende kwa kasi,sisi hatujakataza kuuza mafuta ghafi nje” amesema.

Amesema Serikali hii itawaunga mkono  wawekezeji hasa wa sekta binafsi tutawatetea na kuwalinda ili kufikisha lengo tulilojiwekea la kujitegemea katika mafuta ya kula hapa nchini.

Kwa upande wake Meneja wa wakulima wadogo wa Pyxus Edwin Shio ametaja changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo wakulima kukiuka masharti yaliyopo kwenye mikataba yao ya kupata kibali cha kusafirisha mafuta ghafi kwenda nje ya nchi.

“Tunahitaji kupeleka mafuta nje kwa ajili ya kupata fedha za kigeni ili kuendeleza uzalishaji wa kiwanda chetu lakini changamoto kubwa tunayoipata utakuta mzigo unakaa bandarini zaidi ya wiki hadi mwezi hivyo inakuwa kikwazo kwetu,tunaomba serikali itusaidie ili tupate export ya mafuta tunayotarajia kupeleka nchini Switzerland,” amesema bwana Shio.