Home Mchanganyiko KIWANDA KIDOGO CHA MTOTO WA MAREHEMU DIDAS MASABURI CHAZINDULIWA RASMI NA DIWANI...

KIWANDA KIDOGO CHA MTOTO WA MAREHEMU DIDAS MASABURI CHAZINDULIWA RASMI NA DIWANI VITI MAALUM ILALA

0

 

Diwani viti maalum manispa ya Ilala Batuli Mbaraka Mziya akizindua saloon pamoja na kiwanda kidogo cha vipodozi  kinachomilikiwa na mtoto wa Masaburi kilichopo Tabata na Mikocheni jijini Dar es salaam.

 

 

 

Vicent Macha Dar es salaam

 


Vijana wanaokabiliwa
na changamoto za mitaji kote nchini wametakiwa kuunda vikundi vya watu watano,
kumi au Zaidi ili kuweza kupata mikopo ya halmashauri ambayo ni asilimia 10 iliyotengwa
kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.

Hayo yameelezwa
na Diwani wa viti maalum Manispaa ya Ilala Mh. Batuli Mbaraka Mziya alipoalikwa
kuzindua saloon pamoja na kiwanda kidogo cha vipodozi cha Dote Naturelz Court
kilichopo Tabata pamoja na Mikocheni jijini Dar es salaam.

Mh. Batuli
amesema kuwa Chuchu Dote amekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwani ameitekeleza
sera serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ya kuanziasha viwanda, Kwani
amejipambanua kuwa mzalendo wa kweli kwa kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

Ameongeza
kuwa vijana wengi waachane na dhima ya kusubiri kuajiliwa na matokeo yake
wawekeze nguvu zao katika kujiajiri kama ilivyo kwa Chuchu Dote leo, Kwani amehitimu
degree yake na kaamua kuachana na mambo ya kutafuta ajira na kuamua kujiajiri
na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzake.

Aidha ameedelea kusisitiza kuwa bidhaa za Chuchu Dote ni
nzuri kwani ni za asili na azichubui Ngozi bali zinaimarisha na kuifanya Ngozi
yako iwe nzuri, pia amependa kuwasihi wakina mama pamoja na wakina baba kutumia
bidha hizo kwani hazina kemikali zozote na zinafaa kwa watu wa aina zote

Kwa upande
wake mmiliki wa Dote Naturalz court Chuchu Dote amesema kuwa kwa Tanzania
atakuwa ni msanii wa kwanza wa vichekesho vya jukwani (stand up comedy) kuweza
kumiliki kiwanda kidogo na pia kuwa na mfanikio makubwa kama haya.

Aidha
amesema changamoto kubwa kwa Tanzania ni kwamba watu wakisikia vitu vya asili
mawazo yao uja kwa watu weusi tu,

“Kwani mtu
unapomwambia bidhaa hii ni asili anakwambia hivyo ni vitu vya watu weusi na
siyo kwa sisi weupe na wanasahau kuwa unaweza kuwa mweupe na ukawa natural kwa
kutopaka vitu vyenye kemikali, hiyo ndio shida kubwa kwa wateja wetu wengi”.
Amesema Chuchu Dote

Bidhaa
zinazotengenezwa na Dote Naturalz ni mafuta ya nywele, mafuta ya ngozi
(lotion), shampuu za nywele na sabuni.
Na vyote ni vya asili vinatengenezwa na vitu vya asili kama maji ya
madafu, nazi, parachichi n.k

Ameendelea
kuwasisitiza watanzania wote kutumia bidhaa za Chuchu Dote kwani zinasaidia
kufanya Ngozi iwe nyororo na nadhifu pamoja na mafuta ya dote yanasaidia kukuza
nywele na kuzipa muonekano mzuri.

Na mwisho amewataka
vijana kujituma ili kuweza kufikia mafanikio wanayoyataka lakini pia kujikita
katika ubunifu ili kuimarisha uchumi wa nchi yetu na kumsaidia Rais wetu katika
kukuza na kuinua sekata ya viwanda.

Diwani wa viti maalum manispaa ya Ilala Mh. Batuli Mbaraka Mziya akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa uzinduzi wa kiwanda kidogo cha Dote Naturalz Court kinachomilikiwa na mtoto wa marehemu Didas Masaburi
Wageni wakifuatilia shughuli ya uindui wa Dote Natural Court.
Mkurugenzi wa Dote Naturalz Court, Chuchu Dote Masaburi akionesha baadhi ya bidhaa zinzotengenezwa katika kiwanda chake kilichopo Mikocheni na Tabata jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa wa Dote Naturalz Court Chuchu Dote Masaburi akielezea baadhi ya bidhaa zinazopatika katika kiwanda chake mapema jana jijini Dar es salaam.
 
Mkurugenzi wa Dote Naturalz akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa waliofika katika shughuli hiyo  ya uzinduzi  Dote Naturalz Court

Baadhi ya bidhaa zinazopatikana Dote Naturalz Court

 

Muonekano wa logo ya dote natural court