Home Biashara MWAMBE AITAKA TBS KUFANYA KAZI KWA WELEDI ILI WENYE VIWANDA WAWEZE KUZALISHA...

MWAMBE AITAKA TBS KUFANYA KAZI KWA WELEDI ILI WENYE VIWANDA WAWEZE KUZALISHA BIDHAA BORA

0

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe wakimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Kemia TBS, Bw.Charles Batakanwa akitoa maelekezo baada ya kufanya ziara katika Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania TBS Jijini Dar es Salaam.

   

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Geoffrey Mwambe akizungumza baada ya kutembelea Shirika la Viwango Tanzania  mapema leo Jijini Dar es salaam.

Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania TBS, wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

*********************************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe amewataka wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania TBS kufanya kazi kwa weledi ili kusaidia na kuilea sekta binafsi kwani ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Ameyasema hayo leo Mhe.Mwambe akiwa katika ziara ya kutembelea Shirika hilo Jijini Dar es Salaam akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe.Mwambie amewasisitiza TBS kujenga mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili kuweza kuunda urafiki mzuri na kufanya biashara kuwa rahisi.

“TBS tujenge mazingira sahihi na rafiki ya kuhudumia sekta binafsi ili kuwawezesha kufanya biashara kirahisi”. Amesema Mhe.Mwambe.

Aidha amewataka TBS kufanya kazi na maafisa biashara ili kufanikisha shughuli za viwango katika ngazi za halmashauri.

Nae Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amesema matumaini yao TBS ifanye kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuwawezesha wenye viwanda kuzalisha bidhaa bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt.Yussuf Ngenya amesema wataendelea kulea sekta binafsi kwa weledi na kuwaongoza ili waweze kuzalisha bidhaa bora.