Home Mchanganyiko RC KUNENGE AJA NA MKAKATI WA KUDHIBITI TATIZO LA UCHAFU WA MAZINGIRA.

RC KUNENGE AJA NA MKAKATI WA KUDHIBITI TATIZO LA UCHAFU WA MAZINGIRA.

0

**************************************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema ni wajibu wa kila mkazi wa jiji hilo kuhakikisha anasafisha mazingira ambapo ameeleza kuwa Mkoa umeandaa Mipango kabambe ya kufanya jiji kuwa Katika Hali ya usafi na kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko.

RC Kunenge amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuitumia Kampuni ya usafi ya JKT kufanya usafi kwenye baadhi ya maeneo ya jiji hilo ambapo pia amezielekeza Manispaa za jiji hilo kuongeza adhabu kwa wanaotapisha maji taka kwenye makazi na mitaro ya Maji ya mvua.

Aidha RC Kunenge amesema mikakati mingine ni uboreshaji wa madampo ya taka, Ujenzi wa Kiwanda Cha kuchakata taka na kugeuza kuwa mbolea, upandaji wa Miti, utunzaji wa bustani na kushirikiana na Wadau wakiwemo Bank ya CRDB kupanda miti na Shirika la Sigara ambalo litatoa mapipa 50 kila mwezi ya kuhifadhi taka.

Hata hivyo RC Kunenge amesema Serikali imedhamiria kupatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, unoreshaji wa huduma za Afya, Elimu, Maji na kuweka mazingira Bora ya biashara.