Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya

Mkoa huo (RCC),  akiongoza kikao cha

kamati  hiyo cha kujadili mambo

mbalimbali ya maendeleo mkoani humo, Desemba 17, 2020. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), wakiwa katika kikao hicho muhimu  amacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),  Yohanes Sanga akitoa taarifa ya maazimio ya RCC.

 

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akiwaasa wajumbe kutekeleza kwa makini Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba hivi karibuni viongozi wa CCM wataanza ziara ya kufuatilia utekelezaji huo

 

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, Sambala Said akielezea umuhimu wa viongozi wa ngazi za juu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi ikiwa ni moja ya mbinu ya kuwajengea uwezo wa kielimu na ufaulu mzuri.

 

 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo  akielezea  kuhusu mfumo wa kutambua rekodi za mapato kupitia mashine za kielectroniki.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Mafuru akielezea jinsi jiji liliyyojipanga

 

 kuongeza mapato kupitia vitegauchumi mbalimbali vilivyoanzishwa na vitakavyoanzishwa

 

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Best Magoma akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe kuhusu sekta ya afya

 

 

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma,  Maria Lyimo akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe

 

 

Munge wa  Chemba, Mohamed Monni akiuliza swali kuhusu vigezo vinavyotumika kusajiri shule.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi,Dk. Fatuma Mganga  akielezea mbinu na mikakati iliyotumika   kuifanya Bahi kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi kimkoa.

 

 

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akishauri Mkoa kuwa na ajenda moja ya kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

 

 

Baadhi ya wana sekretarieti ya RCC wakiwajibika

 

 

Wajumbe wa RCC wakifuatilia kwa makini mwenendo wa kikao hicho

 

 

 

 

Na Richard Mwaikenda, CCM Blog Dodoma

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya

Mkoa huo (RCC),  ameongoza kikao cha

kamati  hiyo ambacho kimejadili mambo

mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Kamati hiyo ya ushauri inashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo

baadhi ya wakuu wa idara wa ofisi ya mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi

watendaji wa halmashauri, wabunge, wenyeviti wa 

halmashauri na baadhi ya viongozi wa taasisi.

Awali wajumbe walithibitisha 

muhtasari wa mambo yote yaliyopitishwa katika kikao kilichofanyika mwaka

jana Desemba 19, 2019

Katika kikao hicho  wajumbe walijadili  mada mbalimbali zilizowasilishwa za jinsi ya

kuboresha sekta ya elimu, sekta ya afya, tathmini ya hali ya chakula na maandalizi

ya kilimo msimu wa . 2020/21.

Pia, wajumbe walipitia 

Mpango wa Bajeti ya mwaka  2019/20

na 2020/21 kufikia Noemba 2020,  Mpango wa

Bajeti  wa mwaka  2019/20 kufikia Novemba 2020 na mwelekeo kwa

mwaka 2021/22, mapato ya ndani ya Halmashauri na matumizi kufikia Novemba 2020.

Aidha,wajumbe walipatiwa taarifa  ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge

na Madiwani  Oktoba 2020, Taarifa ya

utekelezaji wa  maazimio ya Kamati hiyo

ya Wakala kwa Huduma ya Misitu (TFS).

Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mahenge ameagiza TFS  kuweka utaratibu wa kukagua mara kwa mara mwenendo

wa upandaji miti katika halamashauri zote ii kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Mkakati huo uhusishe viongozi wa ngazi zote, wakiwemo wakuu wa wilaya,

wakurugenzi wa halmashauri na viongozi wa mkoa.

Baadhi ya maagizo yaliyotolewa kwenye kikao ni; kuunda

Kamati ya Mkoa ya kufuatilia uboreshaji wa 

elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa Mkoa huo ambao kwa hivi sasa

unashika nafasi ya 22 kitaifa.

Dkt. Mahenge amewataka viongozi  wote 

wajenge umoja na ushirikiano kwa kuweka misingi imara ya kudumu  ya kuinua kiwango cha elimu ambayo ni

ufundishaji bora, usimamizi, ufuatliaji na utawala.

Halmashauri zimetakiwa kuandaa vivutio vya uwekezaji,

kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji  na

kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya ardhi kwa wawekezaji na hata

ikiwezekana kuingia ubia nao.