Waziri mteule wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Mwambe (Mb) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Ushindani, Godfrey Machimu mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Ushindani katika Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania, yanayofanyika kuanzia tarehe 3-9 Disemba 2020 Katika uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere Dar es Salaam.
****************************************
Waziri Mteule wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe (Mb) ameipongeza Tume ya Ushindani kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa kunakuwa na Ushindani halali katika biashara na bidhaa bandia sokoni zinadhibitiwa.
Pia ameitaka iongeze juhudi katika kufanyakazi na kujitangaza ili kuongeza kasi katika kukuza Uchumi wa nchi yetu.