Mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini akiwa na Mbunge wa viti maalum CCM Mariam Ditopile wakisubiria matokeo ya uchaguzi wa Jimbo hilo kabla hajatangazwa kuwa mshindi wa CCM wa jimbo hilo.

Msamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini Wakili Msekeni Mkufya akitangaza matokeo ya Jimbo hilo huku  Antony Mavunde  wa Chama cha Mapinduzi akiibuka kidedea kwa kutetea kiti cha ubunge kwa kushinda  kwa kupata kura 86,656 akifuatiwa na Aisha  Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589.

Msamizi wa Uchaguzi jimbo la Dodoma Mjini Wakili Msekeni Mkufya akikabidhi cheti cha ushindi wa Jimbo hilo  Antony Mavunde  wa Chama cha Mapinduzi kuwa mshindi wa Ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 86,656 sawa na asilimia 86.44 akifuatiwa na Aisha  Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589 sawa na asilimia 13.50 

Mbunge Mteule wa Jimbo la Dodoma Mjini  Antony Mavunde  wa Chama cha Mapinduzi akionyesha cheti cha ushindi baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 86,656  akifuatiwa na Aisha  Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Dodoma Mjini  Antony Mavunde  wa Chama cha Mapinduzi akitoa neno la shukrani kwa wanadodoma baada ya kumuwezesha kuibuka mshindi kwa kupata kura 86,656  akifuatiwa na Aisha  Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589.

……………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Msamizi wa Uchaguzi jimbo la Dodoma Mjini Wakili Msekeni Mkufya amemtangaza Antony Mavunde  wa Chama cha Mapinduzi kuwa mshindi wa Ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 86,656 sawa na asilimia 86.44 akifuatiwa na Aisha  Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589 sawa na asilimia 13.50 

Wakili Mkufya amesema kuwa Jumla ya wananchi 335,324 waliojiandikisha huku waliopiga kura ni 102,769.