Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akiongoza kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichofanyika kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu utekelezaji wa mipango ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto katika Ukumbi wa hoteli ya Flomi Mkoani Morogoro Oktoba 21, 2020.Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akichangia jambo wakati wa kikao Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kilichofanyika ukumbi wa mikutano hoteli ya Flomi Morogoro
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao.
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia taarifa za utekelezaji wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakati wa kikao hicho.
Mratibu wa Taifa wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Bi. Happiness Mugyabuso akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Beatrice Mpangala akizungumza masuala ya kisheria wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Wizara ya Kilimo Bw. Philbert Lutale akichangia masuala ajira wakati wa kikao cha kamati elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu (wa pili kutoka kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) mara baada ya kumaliza kikao hicho Mkoani Morogoro.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)