Home Biashara MATUKIO KATIKA PICHA: NAIBU KAMISHNA MKUU TRA AENDELEA NA ZIARA DODOMA

MATUKIO KATIKA PICHA: NAIBU KAMISHNA MKUU TRA AENDELEA NA ZIARA DODOMA

0

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TRA Mkoa wa Dodoma na watumishi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali. Msimamizi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Elisamaria Emmanuel akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kituo hicho kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika ukusanyaji mapato ya Serikali. Msimamizi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Elisamaria Emmanuel akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kituo hicho kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika ukusanyaji mapato ya Serikali.Afisa Msimamizi wa Kodi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mohammedy Madebe akichangia hoja wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akisaini kitabu wa wageni kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa wakati alipomtembelea Katibu Tawala huyo ofisini kwake.  

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akizungumza na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Bi. Sarah Komba wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipomtembelea ofisini kwake ambapo alimshukuru kwa ushirikiano unaotolewa na uongozi mzima wa wilaya hiyo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.  

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Bi. Sarah Komba akizungumza na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipomtembelea ofisini kwake.   Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Mpwapwa Bw. Nelson Makweta akiwatambulisha watumishi wa TRA wilayani humo wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipowatembelea kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.Afisa Msimamizi wa Kodi wa Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Mpwawa mkoani Dododma Bw. Hezekia Shekyandumi akichangia hoja wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)