Home Biashara NAIBU GAVANA BOT KUZINDUA TAWI LA MUCOBA PLC KESHO IRINGA MJINI

NAIBU GAVANA BOT KUZINDUA TAWI LA MUCOBA PLC KESHO IRINGA MJINI

0

Jengo ambalo benki ya Mucoba Plc ipo na kufanyika uzinduzi wake siku ya kesho iringa mjini.

……………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
NAIBU gavana wa benki kuu Tanzania Dkt. Bernard Kibesse kesho jumamosi asubuhi  anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tawi la benki ya MUCOBA PLC tawi la Iringa mjini liloko katika jengo la Motto Family.
Akizungumza na mwanahabari ,Mkurugenzi wa benki hiyo, Philipo Nshokigwa alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa benki hiyo siku ya kesho yamekwisha kamilika na kinachosubiriwa ni uzinduzi wa tawi hilo ambapo limehamia jengo jingine la Motto Family kutoka jengo la Imucu ilipokuwepo awali.
Nshokigwa ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo ambapo wananchi wanaruhusiwa kufungua akaunti kwenye benki hiyo wakati wa shughuli za uzinduzi zikiendelea.
Alisema kuwa uzinduzi wa tawi hilo unafanyika kuweza kuendeleza fursa za kiuchumi  kwa wananchi wa mkoa wa Iringa na mikoa jirani hivyo kurahisisha uwekaji wa kifedha na kukopa kutoka benki hiyo.
Alisema kuwa benki ya Muccoba ina matawi ndani ya wilaya ya Mufindi na wilaya ya Iringa vijiji katika jimbo la Ismani ambapo hifadhi ya taifa ya Ruaha ipo hivyo wanakusudia kupeleka tawi katika eneo la Ruaha ili kuwa karibu zaidi na watalii ambao wamekuwa wakiongezeka kwa lengo la kuwarahishia zaidi huduma za kifedha kwa kutumia benki ya MUCCOBA PLC.
Nshokigwa  alisema kuwa kwa kupitia fursa zilizoko mkoa wa Iringa za kiuchumi benki hiyo imeona vyema kuwasogezea huduma wateja wao kuanzishia mikopo mbalimbali ikiwemo ya elimu,biashara, watoto na akaunti maalum ambazo zinafanya kazi katika benki hiyo
Alisema kama anavyosema Mhe Rais Magufuli anataka wananchi wake wawe na raha kutokanana na fursa zote zinazopelekea kubadilisha maisha yao, hivyo kupitia Benki hiyo ipo kuwasaidia wananchi katika kufikia dhana ya uchumi wa viwanda kwa kusaidia kuongeza dhamana ya mikopo wanayoitaka katika mabenki.
Amewashauri wajasiriamali wadogo na wa kati kuzitumia vema fursa mbalimbali za mikopo kwa wafanyabiashara zilizopo ndani ya Benki ya Muccoba Plc ili kukuza biashara zao kwa lengo la kukuza kipato cha mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.