Martha Petro akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Kombe la ushindi wa Mashindano ya Miss Korosho yaliyofanyika wakati wa Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma Agosti 2020. Kombe hilo alikabidhiwa siku ya kilele cha maonesho hayo Agosti 8, 2020.
Katika Clip hii ya Video, Miss Korosho anaelezea historia ya maisha yake, jinsi alivyoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo na matarajio yake ya baadaye.
Kwa heshima Martha mtoto wa kisukuma akipokea kwa heshima na unyenyekevu Kombe la Miss Korosho kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Nchimbi.
Martha akiwa na furaha mara baada ya kupokea kombe la ushindi.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM