…………………………………………………………………..
Zaidi ya Bilioni 3 zinakusanywa kila mwaka katika Pori la Akiba la Lukwati/Piti lililopo Mkonia Songwe chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA), ambapo ni miongoni mwa mapori ya akiba 23 yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa pori hilo Bw. Jembe Chifuno mbele ya Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania-TAWA Bw. Mabula Misungwi akiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi katika kukagua mapori yanayosimamiwa na TAWA.
Aidha Bwana Chifuno memueleza kaimu Kamishna Mabula kuwa pori hilo lina vivutio vingi vya utalii wakiwepo wanyamapori mbalimbali ambao ni kivutio kikubwa cha wageni wengi kutoka nchi mbalimbali duniani kote kuja kujionea wanyama hao.
Hata hivyo Shughuli za uwindaji ndio sababu kubwa iliyosababisha Pori hili kuwa kinara wa ukusanyaji wa mapato, ambapo mwaka 2018 pori liliingiza Jumla ya Dola za kimarekani 550,000 sawa na Tshs billioni 1.2 na mwaka 2019 ,waliingiza Dola 632,000 sawa na Tshs. billioni 1.4.
Nae Kamishna Mabula Misungwi baada ya kuelezwa hayo alionesha kufurahishwa na kuridhishwa na jitihada zinazofanywa na watumishi wa pori hilo katika kutunza, kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa walizopewa kuzisimamia
Awari Wakizungumza mbele ya Kaimu Kamishna huyo watumishi wa pori hilo walishauri mambo mbalimbali ikiwemo Kuanzishwa kwa utalii wa picha kwani yapo maeneo mengi rafiki kwa aina hiyo ya Utalii.
Mengine ni kugawanywa kwa Pori katika Kanda kurahisisha utekelezaji mzuri wa majukumu yao kwani pori lina ukubwa wa Kilometa za mraba 6,113 ambazo ni kubwa Sana kiutendaji,Waliomba waongezewe vitendea kazi kama vile magari ya doria,mahema na doria za anga kwa kutumia ndege za TAWA na Kuongeza idadi ya watumishi.
Akijibu changamoto za watumishi hao Kaimu Kamishna Mabula aliwapongeza watumishi kwa juhudi kubwa walizofanya kulisafisha pori kwa kuimarisha ulinzi na kuwataka waongeze juhudi na kuahidi kushughulikia changamoto zaidi kadri wawezavyo ili kuongeza morali ya watumishi na mapato