Home Biashara MJENGONI CLASSIC BAND KUSIMAMISHA MJI WA TABORA

MJENGONI CLASSIC BAND KUSIMAMISHA MJI WA TABORA

0

wanamziki bendi ya mjengoni classic band wakiongozwa na Rais wao Digital Mukongya (TIGER)wakiwasha Moto katika ukumbi wa Hugo’s mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki hii(picha na Woinde Shizza )

**************************************

Na Woinde Shizza, michuzi  TvArusha
Bendi maarufu hapa nchini inayojulikana kwa jina la  mjengoni   Classic band yenye makazi yake mkoani Arusha inatarajia kutua mkoani Tabora kutoa burudani katika ukumbi wa Club Inferno  mapema  September 25 na 26 mwaka huu
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdeme alisema kuwa bendi hiiyo inatarajia kusimamisha mji huo na wapenzi wao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo .
Alisema kuwa wamejipanga vyema kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa mkoa huo mzima pamoja na mikoa jirani  na kwa upendeleo watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali  ambazo wameziandaa na zinazotamba kwa sasa .
Alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi itakayo wafurahisha wakazi wa  mkoa mzima kwani hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii ya mjengoni  kutoa burudani mkoani hapo .
Kwa upande wake Rais wa bendi hiyo Digital Mukongya (TIGER) alisema  kuwa atawapa staili zote za bendi hiyo  ikiwemo ile ya   bichwa kubwa   ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.
“tunatarajia kufanya show  ya kihistoria ambayo aijawai kufanyika au kufanywa na bendi yeyote ile  mkoani Tabora  yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya mjengoni classic bandi”alisema Digital
Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa wapenzi wake wa mkoa wa huo  pamoja na mikoa jirani kwani watamuoana namna nyimbo zao zinavyochezwa ikiwemo kuwaona wanenguaji wao namna wanavyojua kulicheza sebene pamoja na kushuhudia namna nyimbo zao zinavyochezwa
“niwaambie tu wakazi wa mkoa wa Tabora kuwa kikosi kizima cha bendi ya mjengoni kitakuwepo na tutatoa buradani ya kufa mtu ,yaani tutatoa burudani zaidi ya tulivyotoa katika mikoa mingine tulioenda kama dar es salaam,Dododa,Mwanza na penginepo nachotaka niwasisitize tu wasiache kuja katika siku hiyo ya shoo waje wajionee burudani ya nguvu”alibainisha Digital