…………………………………………………………………..

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya waajiri wasiozingatia Sheria za Kazi kwa makusudi kwa kisingizio kwamba hawawajibiki chini  ya Sheria hizo. Waajiri hao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa Maafisa  Kazi wanapotekeleza majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za  Kazi katika maeneo ya kazi. Aidha, waajiri hao wamekuwa wakitoa  taarifa potofu kwa Umma, Viongozi wa Serikali na Wanajumuiya wao  kwa lengo la kudhoofisha juhudi zinazofanywa na Serikali katika  kuhakikisha kuwa Sheria za Kazi zinafuatwa na kuzingatiwa nchini.  Ninapenda kuwakumbusha na kuwasisitiza waajiri wote kwamba  wanapaswa kuzingatia na kutekeleza matakwa ya Sheria za Kazi.  

Ninatoa rai kwa waajiri wote nchini kutoa ushirikiano kwa Maafisa Kazi  wanapotekeleza majukumu yao ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za  Kazi. Aidha, iwapo kuna changamoto yoyote katika utekelezaji wa  Sheria, ninawasihi kuwasiliana na Ofisi yangu badala ya kutoa taarifa  potofu kwa Umma, Viongozi wa Serikali na Wanajumuiya wao. 

Ninaomba kuwahakikishia waajiri wote kuwa, Serikali yetu inathamini  Sekta zote ikiwemo Sekta Binafsi na Sekta ya Umma pamoja na  Uwekezaji unaofanywa nchini kwa ustawi wa Taifa letu. 

IMETOLEWA NA 

JENISTA J. MHAGAMA (MB) 

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,  KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU 

19 SEPTEMBA, 2020