Home Uncategorized JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU (21) KWA TUHUMA ZA...

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU (21) KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO NA KUTISHIA UVUNJIFU WA AMANI

0

************************************

TAREHE 20.08.2020 MAJIRA YA 13:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA PASIANSI OFISI YA CCM (W), ILEMEMLA, MKOA WA MWANZA, WATU 21 WANAODAIWA KUWA SEHEMU YA MGOMBEA AMBAE HAKUPITISHWA NA KIKAO CHA KUTEUA MGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CCM KATA YA NYAMANOLO KIKUNDI HICHO KILIFIKA ENEO LA OFISI HIYO KIKIWA KATIKA MAZINGIRA YA KUFANYA FUJO NA KUTISHIA UVUNJIFU WA AMANI ENEO HILO HUKU WAKIWEPO BAADHI YA VIONGOZI WA CCM WANAOFANYA KAZI KATIKA OFISI HIYO.

MARA BAADA YA POLISI KUFIKA ENEO LA TUKIO MTU ANAYEDAIWA KUJULIKANA KWA JINA LA ABRAHMAN KHALFAN KANGE NA ALIYESHIKA NAFASI YA PILI KWENYE

KURA ZA MAONI ZA CHAMA HICHO ALIKIMBIA LAKINI KUNDI ALILOKUA ANALIHAMASISHA KUFANYA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI WA ENEO HILO WAMEKAMATWA, WANAHOJIWA KWA KINA NA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA ILI KUKOMESHA TABIA NA MTINDO UNAOTAKA KUZUKA WA BAADHI YA WAGOMBEA WA VYAMA MBALIMBALI AMBAO HAWAKUPATA FURSA YA KUPITISHWA KUGOMBEA KATIKA VYAMA VYAO KUGEUKA NA KUANZA KUHAMASISHA WATU / VIJANA KUANZISHA VITENDO VYA VURUGU, FUJO SUALA AMBALO NI KOSA KISHERIA NA HALIWEZI KUPEWA NAFASI NA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA  KUFUATILIA KWA KARIBU SHUGHULI ZOTE ZINAZO HUSIANA NA MASUALA YA UCHAGUZI NA LINAWASHUKURU WANANCHI KWA USHIRIKIANO MZURI WANAOUTOA NA KUSISITIZA WASIFUMBIE MACHO VITENDO VYA UHALIFU BALI WAENDELEE KUTOA TAARIFA ILI ZIWEZE KUFANYIWA KAZI HARAKA  NA MWANZA IENDELEE KUWA SALAMA.