Na
mwandishi wetu, Nanyumbu
KAMPENI
ya kuhamasisha wanachi kutumia nishati ya umeme inayoratibiwa na idara ya
masoko ya SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO makao makuu imetua mkoani Mtwara.
Maafisa
wa TANESCO wakiongozana na Meneja wa TANESCO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara,
Mhandisi Sidala Maeda wametembela vijiji kadhaa vikiwemo vya Liputi, Raha leo na Namyomyo na baadaye timu iliungana
na Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Peter Mwaimu na kufika
vijiji vya Tuungane, Mtalikachao
Timu
hiyo ikiwa kwenye vijiji hivyo ilifanya mikutano na wananchi na kutoa elimu kuhusu
matumizi bora na sahihi ya umeme, faida itokanayo na nishati ya umeme ikiwa ni
pamoja na kuwahamishwa wanachi kutumia nishati hiyo kujiletea maendeleo.
“Lakini
pia tumetoa elimu ya jinsi ya kuwaunganishia umeme wana vijiji katika wilaya
hizo kwa gharama nafuu ya Shilingi elfu ishirini na saba tu ( 27,000/=).”
Alisema Mhandisi Maeda.
Alisema wananchi wote wataunganishiwa umeme kwa wakati hivyo basi aliwasisitiza kufanya mtandao (wire
ring) ndani ya nyumba zao kwa
kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa na kuepuka vishoka.
Wilaya
ya masasi pekee ina jumla ya vijiji 67 kati ya vijiji hivyo 43 tayari vineshanufaika
kwa kuwashiwa umeme.
Kwa
upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Nanyumbu Bw. Peter Mwaimu licha ya
kuwahamasisha wananchi kutumia nishati ya umeme lakini pia amewaelimisha kuhusu
matumizi salama ya umeme ili kuepuka athari za matumizi umeme yasiyozingatia
usalama.
Afisa Masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi (kulia) akielezea wananchi wa Tuungane kifaa cha UMETA au umeme tayari ambacho hutumika badala ya wiring, wale ambao hawatafanya wiring watumie kifaa hicho |
Afisa masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi akielezea taratibu za kuunganishiwa umeme kwa kwa gharama nafuu ya Shilingi 27,000/= tuu na kuwashauri wananchi kutumia wakandarasi waliosajiliwa katika Kijiji Cha Raha leo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara