WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 28 ya wiki ya
unyonyeshaji duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani
Muheza
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana Leyna akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata
utepe kuzindua kitini cha lishe ya wanawake,watoto na vijana balehe
wakati wa maadhimisho hayo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
kushoto akimkabidhi Mwakilishi wa Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga
Burhan Yakub kitini cha lishe ya wanawake,watoto na vijana balehe wakati
wa maadhimisho hayo kwa ajili ya waandishi wa habari
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
kushoto akisoma vipeperushi mbalimbali kwenye banda la worldvision
wakati wa maadhimisho hayo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akisalimiana na watu mbalimbali wakati alipowasili kwenye viwanja vya
Jitegemee
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
katika akiwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa maadhimisho
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
TAKWIMU
za hali ya ulishaji watoto nchini zinaonyesha idadi ya watoto
wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee nchini bila kupewa maji, vinywaji
na vyakula vyengine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya
kuzaliwa ni asilimia 58.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa
ufunguzi wa maadhimisho ya 28 ya unyonyeshaji duniani iliyofanyika
kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza.
Ambapo alisema pia
watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi
katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53.
Waziri
Ummy alisema idadi yao wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza kwa wakati
sahihi katika umri wa miezi sita hadi nane ni asilimia 87
“Lakini
pia idadi watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula
kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 36 vigezo hivyo ni
idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake na
uwe na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne
ya vyakula”Alisema
Alisema ili kuboresha viwango vya
unyonyeshaji na ulishaji watoto vyakula vya nyongeza ,kila mmoja ana
wajibu wa kufanya jambo Fulani katika azimio la Inocenti la mwaka 1990
nchi zilikubaliana mambo mbalimbali ya kuyasimamia makubaliano.
Alieleza
kwamba makubaliano hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa zahanati, vituo
vya aafya na hospitali zinazotoa huduma za ukunga zinatoa huduma bora za
kufanikisha unyonyeshaji maziwa ya mama.
Alizitaja baadhi ya
hizo ni pamoja na kutoa elimu ya unyonyeshaji na lishe ya watoto kwa
jamii lakini pia kuhakikisha wanawake wanaojifungua waanze kuwanyonyesha
watoto wao mapema ndani ya saa moja baada ya kujifungua.
“Lakini
pia kuwafundisha wanawake waliojifungua jinsi ya kumpakata na kumweka
vizuri mtoto kwenye titi baada ya kujifungua na jinsi ya kukamua maziwa
ya mama”Alisema Waziri Ummy.
Awali akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe
Tanzania Dkt Germana Leyna alisema kila mwaka dunia nzima inasheherekea
wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Alisema shehe hizo
zilianza rasmi 1991 na nchi iliridhia na kuona ni jambo nzuri lengo
kubwa la wiki hii ni kuhamasisha wakina mama kuwanyonyesha watoto chini
ya miezi sita maziwa ya mama pekee.
Dkt Germana alisema
wanahamasisha jambo hilo kwa sababu maziwa ya mama yanampa mtoto
virutubisho vyote vya lishe anavyohitija kwenye miezi sita ya awali.
Maadhimisho
ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka 2020 yamebabwa na kauli mbiu
inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na
ulinzi wa mazingira”