Home Uncategorized TAKUKURU SHINYANGA WAREJESHA MAMILIONI YA WASTAAFU

TAKUKURU SHINYANGA WAREJESHA MAMILIONI YA WASTAAFU

0

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga  Bw. Mussa Mzee Hussein akiwa tayari kuwasilisha fedha iliyorejeshwa na wafanyabiashara ya ukopeshaji fedha mkoani Shinyanga kwa wasataafu watano mapema jana mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akikabidhi fedha kwa Mwalimu Mstaafu Bw. Elias Katinda zilizorejeshwa na TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga baada yakuwa amepatiwa mikopo umiza kutoka makapuni mbalimbali ya biashara ukopeshaji.

Mwalimu Mstaafu Bw. Elias Katinda akiesabu fedha zake zilizorejeshwa na TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga baada yakuwa amepatiwa mikopo umiza kutoka makapuni mbalimbali ya biashara ukopeshaji.

……………………………………….

Na Mwandishi wetu Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amekabidhi kiasi cha Shilingi M. 42.3 zilizorejeshwa na TAKUKURU Mkoani Shinyanga mali ya wastaafu watano ambao awali walikopa kwa nyakati tofauti toka kwa watu binafsi wenye biashara ya ukopeshaji fedha binafsi na kuwataka wastaafu kote nchini kukopa katika Taasisi za fedha zinazotambulika kisheria.

Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha shilingi M. 110.7 ambazo wakopeshaji hao wanatakiwa kurejesha na Mkuu wa Mkoa amewataka TAKUKURU kuhakikisha fedha zinazodaiwa zinarejeshwa kwa wakati kwa lengo la kuhakikisha haki ya wastaafu hao inatendeka na kuwataka wastaafu hao kuweka fedha zao Benki ili kuepuka kutapeliwa tena.

Bi. Telack pia amewataka TAKUKURU Mkoani Shinyanga kuhakikisha wahusika wote walioshiriki kutapeli fedha ya wasataafu hao wanafikishwa katika vyombo vya dora na kuhagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Shinyanga kushirikiana na TAKUKURU kutekeleza agizo hilo.

‘’Hawa ni Wastaafu tayari wameisha itumikia serikali, nawashangaa vijana ambao wanaibia wazee wenye zaidi ya miaka 60 jambo hili halikubaliki pamoja na kwamba wamerejesha fedha hizi wachukuliwe sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya kazi hizi kwa lengo la kutapeli.’’Aliongeza Bi. Zainab Telack.

Aidha Bi. Zainab Telack amesema kuwa wakopeshaji wengine wanapotakiwa kuweka kiwango cha riba katika mikataba yao wamekuwa hawako tayari kusema kiwango hicho lakini wamekuwa wakisainisha fedha nyingi ambazo mteja anatakiwa kurejesha kinyume na makubaliano.

‘’Mteja anakopa kiasi cha shilingi Milioni mbili lakini katika nakara ya mkataba anaobaki nao mfanyabiashara anaongeza tarakimu ili isomeke milioni 20 hivyo mteja kulazimika kurejesha kiasi kikubwa cha fedha tofauti na makubaliano yake na mteja.’’Alisema Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack.

Naye Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bw.Mussa Mzee Hussein amesema Taasisi yake itajielekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wafanyabiashara na watumishi wa wauma kutojielekeza katika makapuni yenye kutoa mikopo umiza na ambayo wamiliki wake wana hulka mbaya.

Aidha Bw. Hussein amesema Taasisi yake itaendelea kupamba na kuzuia wale wote wanaoendelea na vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanakomesha kabisa ikiwemo kuwachukulia hatua za kisheria kama hawatajiepusha na utoaji mikopo ya chapuchapu ambayo inalenga kutapeli waombaji wa mikopo hiyo.

Mmmoja wa waathirika wa Mikopo umiza ambaye amerejeshewa kiasi cha shilingi M. 18 Mwalimu Mstaafu Elias Katinda amesema kuwa kitendo cha kurejeshewa fedha zake ameamini kuwa kumbe kwa sasa kuna serikali inayojali wananchi wake na kwamba ana imani kubwa na TAKUKURU.

TAKUKURU itaendelea na zoezi la uchunguzi ili kuwabaini wote wealiochukua fedha za wastaafu lakini pia kuwafungulia mashitaka ili iweze kuwa fundisho kwa watu wengine wenye niambaya ya kuendelea kuwatepeli wastaafu kupitia mikopo umiza.