Home Mchanganyiko KLABU YA WAANDISHI MKOA WA MBEYA IMEFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA

KLABU YA WAANDISHI MKOA WA MBEYA IMEFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA

0

Mwenyekiti MBPC BwFesto Sikagonamo akizungumza katika uchaguzi wa viongozi watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Makamu Mwenyekiti MBPC, Bw.Joseph Mwaisango akizungumza katika uchaguzi wa Viongozi watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Viongozi na baadhi ya wanachama MBPC wakipata picha ya pamoja baada ya kufanya uchaguzi wa viongozi watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

**********************************

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC) imefanya uchaguzi wa viongozi wake wataoongoza kwa kipindi cha miaka mitano ambapo Festo Sikagonamo amechaguliwa Mwenyekiti kuiongoza klabu hiyo.

Kamati iliyochaguliwa kusimamia uchaguzi iliongozwa na Ezekiel Kamanga,Esther Macha na Yonathan Kossam.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi katika ukumbi wa Elimisha Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Ezekiel Kamanga alimtangaza Joseph Mwaisango kuwa Makamu Mwenyekiti.

Keneth Mwakandyali amechaguliwa kuwa Katibu wakati Mtunza Hazina akichaguliwa Lukia Chasanika.

Wajumbe watatu wanaoingia Kamati Tendaji ni pamoja na Elizabeth Nyivambe,Grace Mwakalinga na Bosco Nyambege.

Kamati ya Mipango na Uchumi amechaguliwa Gabriel Mbwile Kamati ya Mafunzo na Ujenzi amechaguliwa Fredy Jackson na Kamati ya maadili amechaguliwa Ezekiel Kamanga.

Kamati ya Mipango na Uchumi,Kamati ya Mafunzo na Ujenzi pia Kamati ya maadili zitachagua wajumbe watatu kila moja kuunda kamati zao.

Awali uongozi wa mpito ulioongozwa na Festo Sikagonamo ulitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ukiwemo mpango kazi wa miaka mitano unaoanisha mipango mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo kongwe ya Waandishi nchini.

Baada ya kumalizika uchaguzi Mwenyekiti Festo Sikagonamo aliwashukuru wanachama kwa kumpa dhamana ya kuwaongoza hivyo wamoja kwa mustakabali wa maendeleo ya wanachama wake.

Grace Mwakalinga aliwaomba wanachama kuondoa tofauti zao ili kuijenga klabu imara.