Home Biashara MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO, WIZARA YA MADINI ATEMBELEA BANDA LA TUME...

MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO, WIZARA YA MADINI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

0

Leo tarehe 11 Julai, 2020 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal ametembelea banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saam.

Mara baada ya kutembelea mabanda na kupata maelezo ya kina kuhusu mafanikio ya Sekta ya Madini amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Madini na Taasisi zake kwenye uelimishaji wa umma kupitia maonesho.

Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali.