Home Biashara TEMESA YASHIRIKI MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

TEMESA YASHIRIKI MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

0

Nahodha wa kivuko Magogoni Kigamboni Shabani Mlangara kushoto akimuelekeza namna ya kutumia kifaa cha kuzimia moto (fire extinguisher) mmoja wa washiriki wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba aliyetembelea banda la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mwishoni mwa wiki hii kujifunza kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala huo katika Maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa kivuko Magogoni Kigamboni Shabani Mlangara kushoto akimpa elimu ya jinsi ya kutumia maboya ya kujiokolea mmoja wa washiriki wa Maonesho hayo aliyetembelea Banda la TEMESA kujifunza kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala huo katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.Maafisa kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiendelea kutoa elimu kwa washiriki kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TEMESA katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Waziri Jumbe kulia akizungumza na  baadhi wa washiriki waliotembelea banda la Wakala huo jana kujifunza kuhusu huduma zinazotolewa na TEMESA katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA TEMESA