Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augistino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka huu 2020.
*********************************
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO,
DAR ES SALAAM
24.6.2020
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour Party, Augustino Mrema amesema chama hicho kinaendelea na msimamo wake wa kumuunga mkono, Rais Dkt. John Magufuli kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, Augustino Mrema alisema kuwa katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano imekilazimu chama hicho kuunga mkono kuwa TLP haitosimamisha mgombea na badala yake Rais Dkt.John Magufuli apitishwe kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais wa Tanzania mwaka huu kwa hoja kuu tano.
“Tanathamini Kazi zinazofanywa na Mhe. Dkt John Magufuli na asilimia 98% ya wajumbe kwenye Kamati Kuu na 100% kwenye Halmashauri Kuu walitoa pendekezo la TLP kutoweka mgombea wa Urais na badala yake chama kimuunge Mkono Mgombea wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mh Dk John Pombe Joseph Magufuli” alisema Mrema
Alisema kuwa katika kutekeleza kazi za maendeleo Uongozi wa Rais Dkt John Pomnbe Magufuli ulishughulikia suala la Watumishi hewa kuwaondoa watumishi wenye dosari wapatao 32,555 sawa na asilimia 5% ya watumishi wote Serikalini na kuokoa pesa Tshs 19.8bln kwa kila mwezi sawaTshs 237.6 bln kwa mwaka.
Alibainisha suala lingine linalofanya TLP kumuunga mkono Dkt John Magufuli ni kuhusu kusambaza umeme wa uhakika mjini na vijiji kitu ambacho siku za nyuma kidogo hakikuwezekana lakini katika utawala wake umeme umefika hadi vijijini
“Wakati Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 palikuwa na vijijini 2,018 tu vyenye umeme kwa lugha rahisi tangu Tanzania ipate uhuru ni vijiji 2,018 tu kati ya vijiji 12,268 sawa 17% ndio vilikuwa na lakini mpaka sasa vijiji 9,112 sawa na asilimia 74.3, ambalo ni ongezeko la vijiji 7,094 sawa na asilimia 57.3”, alibainisha Mrema.
Aliongeza kuwa katika sekta ya ujenzi wa Miundombinu Serikali ya Dkt.John Magufuli imejikita katika kubadilisha mandhari ya Tanzania katika Majiji, Miji na vijiji mabili mbali.
Alisema kwa upande wa miradi, Tanzania imeendelea kufanya vizuri, huku akitolea akilitaja jarida la The Africa Construction trend report 2019” linaloonyesha jumla ya miradi 51 ya Tanzania ikiwa na thamani ya thamani ya Dola za Marekani Bilioni 60.3 ya thamani ya miradi yote.