Home Biashara TECNO YAZINDUA RASMI SPARK 5 SIMU YENYE KAMERA 5

TECNO YAZINDUA RASMI SPARK 5 SIMU YENYE KAMERA 5

0

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imetangaza rasmi kuzindua simu yake mpya TECNO SPARK 5 yenye kamera tano ambapo uzinduzi huo umefanyika Jijini Dar es Salaam moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii zikiwemo kurasa za mitandao ya kijamii za TECNO.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed alisema uzinduzi wa simu hiyo umekuja ukiwa umeambatana na kifurushi cha zawadi kwa wateja yaani (Gift Box) ambayo ni maalum kwaajili ya mteja yeyote anayenunua TECNO SPARK 5.

“Tumekuja na vitu spesho sana kwaajili ya wateja wetu tuna zawadi nyingi sana tofauti tofauti ambazo mteja wetu yeyote wa TECNO SPARK 5 atakutana nazo na hapa kuna Gift Box na ndani yake kuna vitu tofauti tofauti zikiwemo kibeba funguo(Key holder), selfie stick,chupa, headphone pamoja na kifuko maalum cha kuhifadhia simu unapokuwa mazoezini” Alisema Bi. Mariam

 

Meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed (Kulia), balozi wa TECNO SPARK 5 Bw. Jonijo (Katikati) na Msimamizi wa duka la TECNO Bi. Evelyn (Kushoto).

Bi. Mariam aliongeza kuwa zawadi hizo zitatolewa kwa mteja yeyote atakayenunua TECNO SPARK 5 na kwamba tayari promosheni hiyo imeanza rasmi nchi nzima katika maduka yote ya TECNO.

Wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya TECNO SPARK 5 inayosifika kwa kamera 5 zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha mahali popote hata gizani, TECNO pia ilimtambulisha rasmi Bw. Jonijo ambaye ni mtangazaji maarufu wa radio, kuwa balozi wa TECNO SPARK 5.

Kwa upande wake balozi huyo wa TECNO SPARK 5 alisema amekuwa mfuatiliaji mzuri wa matoleo ya TECNO SPARK, kuanzia SPARK 3, SPARK 4 mpaka sasa SPARK 5.

“Mchongo wa TECNO SPARK 5 umekaa poa sana, unajua TECNO sasa hivi wamerahisisha maisha kwasababu SPARK 5 kuna kioo nimekutana nacho kina maajabu yaani ni inchi 6.6”, SPARK 5 pia ina kamera 5 kwaajili ya picha na video kali wakati wowote” Alisema Jonijo

Bw. Jonijo, balozi wa TECNO SPARK 5

“Unajua kamera hizi zinavyofanya kazi hata lile tone la maji unaweza kulinasa kwa kamera ya TECNO SPARK 5, na kitu kizuri zaidi betri yake ni 5000mAh hiki kitu ni balaa habari ya kuchaji simu kila siku sahau, hii ukichaji mara moja unakwenda nayo siku 3” Aliongeza Jonijo.

Afisa masoko mitandaoni wa TECNO Bi. Salma Shafii (Kulia) akiwa na Balozi wa TECNO SPARK 5, Jonijo.

Tayari TECNO SPARK 5 ipo kwenye maduka ya simu mikoa yote Tanzania bara na visiwani huku bei yake ikiwa ni rafiki katika kipindi hiki. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania.