Home Biashara TBL Plc yatoa msaada wa vitakasa mikono mkoani Mwanza

TBL Plc yatoa msaada wa vitakasa mikono mkoani Mwanza

0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella (aliyevaa miwani) akipokea moja ya vidumu vya vitakasa mikono(Sanitizer) kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha bia cha TBL tawi la Mwanza, Patel Kilovele, kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza, TBL imetoa lita 500 za Sanitizerkupambana na maambukizi ya Covid 19(kulia)ni Katibu Tawala wa mkoa huo Emmanuel Tutuba akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongella,akiongea baada ya kupokea vitakasa mikono kutoka kwa Mènera wa TBL Mwanza,Patel Kilovele.

******************************

 Katika jitihada za kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kukabiliana na maambukizi yavirusi vya COVID-19 nchini, Kampuni ya bia ya TBL Plc , imetoa msaada wa lita 500 za vitakasa mikono kwa ajili ya matumizi kwenye vituo vya afya mkoani Mwanza.

Meneja wa kiwanda cha TBL kilichopo mkoani MwanzaPatel Kilovele,,amesema kuwa kampuni kama mdau wa kuzalisha vinywaji vikali ambavyo moja ya malighafi zake zinatumika kutengeneza vitakasa mikono imejitoa katika kipindi hiki kuhakikisha inaunga mkono jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa kuzalisha na kutomsaada wa bidhaa hizo.

Aliongeza kusema kuwa kampuni inaamini kuwa kuwepo kwa jamii yenye afya njema na mazingira tulivu ni muhimu kwa taifa.  Alishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya kupambana na ugonjwa wa COVID 19 na kuongeza “Tutaendelea kujitoa katika kukabiliana na janga hili kama ambavyo leo tumetoa vitakasa mikono kwa ajili ya kutumika katika vituo vya afya” alisema Ayo. 

 Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliishukuru kampuni hiyo kwa kusaidia vituo vya afya mkoani humo na kuwataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa COVID 19 nchini.