Home Uncategorized THBUB IMETUMA SALAM ZA POLE KWA RAIS MHE. JOHN MAGUFULI KUTOKANA...

THBUB IMETUMA SALAM ZA POLE KWA RAIS MHE. JOHN MAGUFULI KUTOKANA NA MSIBA WA BALOZI DKT.AUGUSTINE MAHIGA

0

***********************************

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) kilichotokea leo alfajiri Mei 01, 2020 Jijini Dodoma.

Tume inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za Kimataifa kwa miaka mingi.

Aidha, Tume inatoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria, familia ya Marehemu na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Tume ikiwa taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria
inaungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu na inawaomba wanafamilia wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi, Amina.