……………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI ,BAGAMOYO
JUMUIYA ya Wanawake Wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani, (UWT),imewataka wanachama wa Jumuiya hiyo kujiandaa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kuanza hivi karibuni ,pasipo kujiweka nyuma.
Katibu wa UWT Bagamoyo, Hanifa Checheta aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilayani hapo, ambapo alisema wakati mchakato wa uchaguzi ngazi za Udiwani, Ubunge ukiwadi ,wanawake wajitokeze kuwania uongozi ndani ya kata na Jimbo hilo .
Alieleza kuwa ,wanawake wanapaswa kuthubutu kugombea bila uoga katika nafasi yoyote na sio tu kukimbilia viti maalum pekee bali hata kata na majimbo.
Hanifa alisema , katika mchakato huo wana-CCM hawana mbadala katika nafasi ya urais, kwani aliyekuwepo hivi sasa Dkt. John Magufuli ameitendea vema haki nafasi hiyo hakuna ambaye haoni juhudi za uongozi wake.
“Nitumie nafasi hii kuwahamasisha,Wanawake kujiandaa na kinyang’anyiro cha Udiwani na Ubunge pindi mida itakapofika kwani nina imani kubwa wanaweza kushika uongozi ngazi hizo,” alisema Checheta.
Akizungumzia janga la ugonjwa wa Corona, Katibu huyo aliwataadhalisha wanawake kuwalinda watoto wakiwa majumbani wasicheze ovyo na kuwajengea tabia ya kupenda kunawa mara kwa mara ili kuwaepusha na janga hilo .
Hanifa anasema ,wakati wa janga kamaa ili umoja unatakiwa kwani ugonjwa hauchagui mwana-CCM wala chama kingine,hivyo kila mmoja ajikinge na awe na tahadhali na ugonjwa huo .