Home Biashara VODACOM YATAMBULISHA PEPPER ROBOT KWENYE MAONESHO YA UBUNIFU DODOMA

VODACOM YATAMBULISHA PEPPER ROBOT KWENYE MAONESHO YA UBUNIFU DODOMA

0

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania , Jacquiline Materu (kulia) akiwapa maelezo baadhi ya wananchi kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper ,walipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknilojia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania ,Jacquiline Materu (kushoto) akimpa  maelezo Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk.Avemaria Semakafu (kulia) na msafara wake kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper ndani ya  banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

Mratibu wa mradi wa Instant Schools ulio chini ya Vodacom Tanzania Foundation,Christine Lucas (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Avemaria Semakafu wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.