Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye hafla ya Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakimsikiliza mgeni rasmi Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Dkt. Eliezer Feleshi (ambaye hayupo pichani).
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati )kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu ya Tanzania ambao ni baadhi yao ni wajumbe wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), (kulia kwake) ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Joaquine De Mello na( kushoto) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Rehema Kerefu.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mahakamani hapo Jijini Dar es salaam (kulia kwake )ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello ambaye pia nia Mwenyekiti wa (TAWJA) na (kushoto )ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Rehema Kerefu.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Joaquine De Mello ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) akitoa mada wakati wa hafla ya kusherekea Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi ya Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu ya Tanzania wakiwa ukumbini wakimsikiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania ( ambaye hayupo pichani) wakati wa hafla ya sherehe ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mahakmani hapo Jijini Dar es salaam wakiongozwa na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Messeka Chaba (wa pili Kushoto).
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu ya Tanzania na Naibu Wasajili ambao ni wajumbe wa Chama TAWJA, (kulia) ni Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Joaquine De Mello, ambaye Mwenyekiti wa TAWJA na (kushoto) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Rehema Kerefu na wa kwanza
kulia waliosimama ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharimillah Sarwatt.
(Picha na Innocent Kansha- Mahakama)
………………………………………………………………………………………..
Na Innocent Kansha – Mahakama
Mahakama ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala mtambuka la kuhusu uwiano sawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika nafasi za kada mbalimbali za Utumishi wa Umma.
Akizungumza jana wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mahakamani hapo Jijini Dar es salaam, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi alipoalikwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).
Katika hafla hiyo, Jaji Kiongozi alizitaja baadhi ya kada ambazo zina asilimia 100 idadi ya wanawake ni pamoja na Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania anayeshughulikia migogoro ya kisheria ikitokea Mahakamani kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kada nyingine, ya Maafisa Utumishin ambayo ina idadi ya wanawake 66 ukilinganisha na wanaume ambao ni 44 sawa na asilimia 58 kati yao.
Aidha, alieleza kuwa kwa upande wa Mahakimu katika Mahakama za ngazi ya chini kama Mahakama za Mikoa na Wilaya mlinganyo wao upo sawa kati yao wanawake ni 467 na wanaume wapo 467 kwa idadi sawa, Mahakama za Mwanzo nchini Mahakimu wanawake ni 147 na wanaume ni 203, Maafisa Ugavi wanawake ni 17 na wanaume ni 14 sawa na asilimia 55, kwa Upande wa Maafisa Habari Wanawake watatu na wanaume wawili sawa na asilimia 60.
Dkt. Feleshi aliwasisitiza Majaji wanawake kutumia muda wao kuendelea kuwafunza watumishi wengine wa jinsia ya kike na kuwaongoza kwa misingi ya utendaji kazi kwa uaminifu, uadilifu, bidii ya kujituma na maarifa.
Aliwataka Majaji na Wasajili wanawake watumie kauli mbiu yake katika kutimiza majukumu yao inayosema “Jaji ni Kiongozi na anao wajibu wa kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/20 na Utawala, kueni na upendo miongoni mwenu, majungu na fitina mahala pa kazi havina nafasi,’’ alisisitiza.
Aliongeza kuwa siku zote duniani mwananamke akifaulu mahali pa kazi panakuwa na ustawi wa hali ya juu, hivyo wakubali kusahishwa pale inapooneka mambo hayaendi sawa ili kuondoa tofauti zao.
Naye Jaji Joaquine De Mello aliwaasa wanawakehao kutokubali kutumika wala kujihusisha na vitendo vya rushwa ya ngono mahala pa kazi kwani vinadhalilisha jinsia ya kike na kuondoa utu wa mwanamke katika eneo hilo.