Home Biashara NMB Mbele Kuhakikisha Upatikanaji wa Usawa kwa Wote

NMB Mbele Kuhakikisha Upatikanaji wa Usawa kwa Wote

0

Tukiadhimisha ‘Siku ya Wanawake Duniani’, Benki ya NMB imekua katika mstari wa mbele kuunga mkono kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani #EachForEqual, ambayo inaangazia Usawa kwa Wote. Katika Maadhimisho yaliyofanyika kitaifa Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu mapema leo, NMB imekua miongoni mwa wadhamini wakuu walionogesha maadhimisho hayo kwa kutoa shilingi
Milioni 26 ambapo pesa taslimu ni milioni 5 pamoja na fulana zenye thamani ya shilingi Milioni
21.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Serikali wa NMB – Vicky Bishubo, alipotembelea banda la benki hiyo mjini Bariadi
Mkoani Simiyu kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Ummy Mwalimu.

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika kitaifa Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu- Antony Mtaka (Kushoto) akifurahia jambo na Mbunge wa Urambo – Margaret Sitta, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB -Ruth Zaipuna na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi- Sospeter Magesse.

Wakiongozwa na Kaimu Mkuruzenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna kwa pamoja wanasema ‘Usawa kwa Wote’

Tunawatakia, kheri ya Siku ya Mwanamke!
#NMBBankKaribuYako