Home Mchanganyiko DC MBONEKO AONGOZA MAMIA YA WANAWAKE KONGAMANO LA WANAWAKE ‘SHINYANGA WOMEN’S DAY...

DC MBONEKO AONGOZA MAMIA YA WANAWAKE KONGAMANO LA WANAWAKE ‘SHINYANGA WOMEN’S DAY OUT’

0


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kongamano la wanawake “Shinyanga Women’s Day Out” lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change kutoka Shinyanga mjini leo Jumamosi Machi 7,2020. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog

Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women’s Day Out wakiwa ukumbini.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women’s Day Out.

Meza Kuu ‘VIP’ wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women’s Day Out.


Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiingia kwenye Kongamano la wanawake Shinyanga, ” Shinyanga Women’s Day Out.”

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wapili kulia, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wanawake na mabadiliko (WCF) wakati alipowasili kwenye Kongamano la wanawake, “Shinyanga Women’s Day Out.”

Baadhi ya wajumbe wa  kikundi na mabadiliko (WFC) wakipiga picha ya pamoja na wawezeshaji wa mada kwenye Kongamano la wanawake kutoka Jijini Dar es salaam, akiwamo Sadaka Candi ambaye ni mwanasaikolojia (wanne kutoka kulia), akifuatiwa na Mchumi Hilda Kisoka mwenye nguo nyeusi.

Mwenyekiti Msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change Getrude Munuo, akitambulisha wajumbe wa kikundi hicho pamoja na kufungua rasmi Kongamano hilo.

Mwenyekiti wa maandalizi wa Kongamano hilo Fausta Kivambe, akitoa shukrani kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na mwenyekiti msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC) Getrude Munuo, wakikata Keki kwa ajili ya kufungua Rasmi Kungamano hilo la wanawake.

Wanawake wa kikundi cha mabadiliko (WFC), Wakifungua Shampeni tayari kwa kuanza kwa Kongamano hilo la Wanawake Shinyanga mjini, “Shinyanga Women’s Day Out.”

Watoa mada wakiwa wameketi kwenye meza tayari kwa kutoa elimu mbalimbali kwenye Kongamano hilo la wanawake Shinyanga “Women’s Day Out.”


Sadaka Candi (Maarufu Ant Sadaka) mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la  wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.

Sadaka Candi( Maarufu Anti Sadaka), mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.


Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la “Shinyanga Women’s Day Out” Shinyanga mjini, lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC), wa pili kushoto ni mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga, na wa kwanza kushoto ni Diwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga Mariamu Nyangaka.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women’s Day Out.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women’s Day Out.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women’s Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women’s Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women’s Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women’s Day Out


Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili kwenye Kongamano la wanawake “Shinyanga Women’s Day Out” kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akipokewa na wanawake na mabadiliko (WFC) ambao ndiyo waandaji wa Kongamano hilo.
Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog

Kongamano la wanawake Shinyanga mjini (Women’s Day Out), lililoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na mabadiliko (Women for Change – WFC ), limehudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka Shinyanga mjini, kwa ajili ya kupewa elimu mbalimbali ikiwamo ya malezi, afya, sheria, pamoja na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 7, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Mboneko aliwataka wanawake Shinyanga mjini washirikiane na kuungana mkono, ikiwamo kwenye masuala ya kuinuana kiuchumi na kuacha tabia ya kutopendana.

Alisema huu ni wakati wa wanawake kushirikiana, kupendana na kuungana mkono kwenye masuala ya kibiashara kwa kununuliana bidhaa, na kuacha tabia kutopendana ili wapate kusonga mbele kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kutumia vyombo vya habari na mitandao ya jamii kutangaza shughuli wanazofanya.

“Napongeza sana kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko cha Women for Change kwa kufanya Kongamano hili la wanawake Shinyanga mjini, na hasa kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni Machi 8,2020  kwa kukutanisha wanawake kupewa elimu mbalimbali kwa mstakabali wa maisha yao,”alisema Mboneko.

“Kupitia Kongamano hili naomba wanawake, mpendane, mshirikiane, pamoja na kuungana mkono kwenye biashara mbalimbali ili mjikwamue kiuchumi, ambapo dhana za kuchukiana zilishapitwa na wakati, kipindi hiki ni cha mabadiliko wanawake tuungane na kuwa kitu kimoja,”aliongeza.

“Pia nakipongeza kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko kwa kufanya ukarabati wa bweni la wavulana kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino Buhangija, ili kuwaweka katika mazingira mazuri, mfano ambao unapaswa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo”,alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko ‘Women for Change, kutoka Shinyanga mjini Getrude Munuo, alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2013 na 2014 walipata usajili, na lengo lao kubwa ni kusaidiana kuinuana kiuchumi pamoja na kufanya shughuli za kijamii.

Alisema wameendesha kongamano hilo kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali kwa wanawake wa Shinyanga mjini, ikiwamo ya malezi, afya pamoja na namna ya kushirikiana kibiashara ili kuinuka kiuchumi.