Home Biashara BASHUNGWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA 10 LA BIASHARA ZANZIBAR

BASHUNGWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA 10 LA BIASHARA ZANZIBAR

0

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Kumi la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe.Dk. Ali Ali Mohamed Shein.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati akilifungua Jukwaa la Kumi la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na kuwashirikisha Wadau wa Sekta Binafsi na za Umma na Wafanyabiashara Zanzibar

BAADHI Wajumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kumi wa Jukwaa la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

……………………………………………………………………………………………

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameshiriki kwenye Mkutano wa Jukwaa la kumi (10) la biashara Zanzibar. Lenye kauli mbiu isemayo “Ushirikishwaji katika kuleta maendeleo endelevu kupitia uchumi wa bahari”

Mkutano huo umefunguliwa Leo 07.03.2020 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa jukwaa la biashara na Rais wa Zanzibar Mhe .Dkt Ali Mohamed Shein ambae amefungua jukwaa hilo ambalo lengo kuu ni kutazama fursa za uchumi wa bluu (Blue Economy) kwa maendeleo ya Zanzibar