Home Mchanganyiko 700 hawajaripoti kidato cha kwanza Njombe

700 hawajaripoti kidato cha kwanza Njombe

0

**************************

NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ameonyesha Kukasirishwa na kitendo cha wanafunzi 708 waliofahuru kidato cha kwanza kushindwa kujiunga na masomo na kutoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji na maafisa elimu kata pamoja na viongozi wa mitaa na vijiji kuhakikisha wanafunzi hao wanajiunga na masomo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Olesendeka ametoa agizo hilo katika kikao cha tathimini ya elimu kilichokutanisha halmashauri zote za mkoa huo na wadau wa elimu ambapo anasema ni jambo la kushangaza kuona wanafunzi wagoma kuendelea na masomo wakati serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuboresha miundombinu ya elimu hivyo zoezi la kuwatafuta na kuwapeleka shule wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza.

Akiweka bayana kuhusu idadi ya wanafunzi waliofauru kidato cha kwanza, walioripoti na ambao hawajaripoti tangu januari 6 shule zilipofungua ,afisa elimu mkoa wa Njombe Gift Kyando anasema takribani wafunzi 15,711 walifauru lakini asilimia 84.7 pekee ndiyo walioripoti shule na kuitaja wilaya ya Ludewa kuwa na wanafunzi 200 ambao hawajaripoti.

Nao baadhi ya wadau wa elimu wakitoa mapendekezo ya kuboresha sekta ya elimu akiwemo Flaten Kwahison, Ewdin Mwanzinga na Joram Hongoli mbunge wa Lupembe wanasema ili mkoa uweze kupiga hatua inapaswa kuboresha mazingira ya kupokea na kutoa elimu ,nidhamu na umoja ambayo utekelezaji wake utafanyika kimkakati wa mda mfupi na mrefu.

Wamesema ili kuwa kinara kataifa katika matokeo ya ngazi tofauti za elimu mkoa kwa kushirikiana na wadau upaswa kuweka mazingira rafiki ikiwemo kujenga nyumba za walimu,madarasa yakiwa na madawati ya kutosha pamoja uwepo wa vitabu vya kiada na ziada

Katika kikao hicho tuzo za fedha na vyeti zimetolewa kwa halmashauri na shule ambazo zimefanya vizuri kitaaluma.