Katibu tawala wa wilaya Arusha,David Mwakiposa akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Meneja wa mradi wa wash SDG Tanzania,Olivier Germain kutoka shirika la SNV(Happy Lazaro).
Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akizungumza katika halfa hiyo ya upokeaji wa vifaa vya utunzaji wa mazingira vilivyotolewa na shirika la SNV(Happy Lazaro).
***********************
Happy Lazaro,Arusha.
Wananchi wa Jiji la Arusha ,wametakiwa kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya usafi ambayo itasaidia kuweza kuepukana na magonjwa ya milipuko.
Hayo yalisemwa Jana Katibu tawala wa wilaya ya Arusha,David Mwakiposa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa Kinga kwa wamiliki wa makampuni yanayofanya usafi wa mazingira Jiji la Arusha vilivyotolewa na shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) iliyofanyika mjini hapa.
Alisema kuwa ,ili wananchi wa Jiji la Arusha waweze kuishi maisha mazuri yenye usalama na Afya nzuri ni jukumu lao kuhakikisha wanayaweka mazingira yao katika hali ya Usafi kila wakati kwa lengo la kuepukana na milipuko ya Magonjwa.
Akaitaka halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha wanasimamia vifaa walivyopewa na wafadhili na vinatumika kwa mahitaji yaliopangwa huku wakihakikisha wanatoa taarifa kila mwezi za waharibifu wa mazingira na hatua zilizochukuliwa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mratibu wa kampeni ya taifa ya Usafi wa mazingira Jiji la Arusha ,Allan Rushokana alisema vifaa kinga hivyo vina thamani ya milion 4.8 na vinatolewa kwa kampuni 7 zinazofanyakazi ya Unyonyaji wa maji taka ndani ya Jiji hilo.
Akatoa wito kwa wananchi kuendelea kutumia huduma hizo kwa lengo la kuhakikisha wanayaweka mazingira yao katika hali ya Usafi itakayosaidia kuondokana na maradhi ya milipuko ambayo yanaweza kuepukika wakitumia huduma za Unyonyaji wa maji taka kwa wakati.
Alisema kuwa Jiji hilo kupitia mradi huo watahakikisha linakuwa kwenye hali ya Usafi wa mazingira na watakuwa wakali pindi watakapoona sheria za mazingira zikivunjwa na kuwataka wananchi kufuata sheria na kuyaweka mazingira katika hali ya Usafi kwa maisha Bora ya kila siku.
Nae Mshauri wa Mradi wa Maji na usafi wa Mazingira Sauli kutoka shirika la Maendeleo ya Uholanzi (SNV),Sauli Mwandosya alieleza kuwa baada ya kufanya utafiti wa kina waligundua kuna changamoto kubwa ya watu kufanya kazi za Usafi wa mazingira bila vifaa ndio maana wakaanzisha utoaji wa elimu na vifaa kwa makampuni ya Usafi wa mazingira Jiji la Arusha kwa lengo la kuondoa changamoto na kuepuka magonjwa.
Naye Mratibu wa programu wa elimu ya Afya mashuleni Jiji la Arusha,Monica Ngonyani alisema kuwa,mradi wa usafi wa mazingira mjini ni mradi unaotekelezwa na halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira (AUWSA)ambapo mradi una huu umejikita katika kuboresha mnyonyoro wa huduma ya usafi wa Mazingira hususani uthibiti wa kinyesi Cha binadamu.
“mradi huu ni wa miaka mitano ulioanza 2017 hadi 2022 na wafadhili wakuu ni kitengo maalumu ndani ya wizara ya mambo ya nje ya Uholanzi,ambapo walengwa wakuu wa kufikiwa na mradi ni kaya,shule,vituo vya kutolea huduma tiba,watoa huduma ya Unyonyaji wa tooe kinyesi ,na vyoo vya umma’alisema Monica.