Mmoja wa Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa Mbeya akisoma ujumbe ambao ametumiwa ambao uanaonyesha ni Uhalifu wa utumiaji huduma za mawasiliano.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi akitoa maelezo kuhusiana na Kujikinga na Uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja katika Semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya
Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Semina ya TCRA ya Kujikinga na Uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Mkuu wa Nyanda za Kusini Asajile John akizungumza na Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya kuhusiana na Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ya Uhalifu katika Semina iliyofanyika jijini Hapa
******************************
Kamati ya Amani mkoa wa Mbeya wameiahidi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)kupeleka elimu ya kujikinga na uhalifu wanapotumia huduma za mawasiliano kwa waumini wao kama walivyoumbwa ili ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa ustawi wa nchi yetu
Viongozi hao
Wameyasema hayo walipokuwa semina ya kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja haingizwi chaka inayolenga katika kuelimisha umma ya kujikinga.
Wakichangia katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda wateja na kuahidi kushiriki katika kampeni hiyo.
Viongozi hao wametoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa TCRA katika kuelimisha umma kwani viongozi wa dini wanawafuasi wengi na ushawishi mkubwa ktk jamii Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu mitandaoni yenye lengo la kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga ili wasirubuniwe wanapotumia huduma za mawasiliano.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali
Nae Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.
Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana sana na teknolojia yake inabadilika kila siku
John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama kwa ustawi wa nchi.
Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanatumia mawasiliano vibaya mkono wa sheria utawakuta.