Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources, Joseph Kimogele (kulia) akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni yake kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) mara alipofanya ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu kwenye kampuni hiyo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020. Wa pili kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Chunya, Godson Kamihanda.
Shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu zikiendelea katika Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources, iliyopo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources, Joseph Kimogele (katikati) akielezea matumizi ya mtambo maalum wa kuchenjua madini ya dhahabu kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( wa pili kushoto) mara alipofanya ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu kwenye kampuni hiyo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020. Kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Chunya, Godson Kamihanda.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources na wataalam kutoka Tume ya Madini mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi kwenye kampuni hiyo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources, Joseph Kimogele (mbele) akielezea matumizi ya bwawa la kuhifadhi mabaki ya udongo wenye madini ya dhahabu uliochenjuliwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini pamoja na timu yake kwenye ziara yake ya kikazi kwenye kampuni hiyo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Apex Resources, Joseph Kimogele (kulia) akielezea namna uchimbaji wa chini ya ardhi unavyofanyika kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) kwenye ziara yake ya kikazi kwenye kampuni hiyo katika eneo la Itumbi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 14 Februari, 2020. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Chunya, Godson Kamihanda.