Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu kwenye wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Mratibu wa Mradi wa EACOP kutoka Wizara ya Nishati, Salum Mnuna(wa kwanza kulia) Kamishna wa Nishati na Gesi Adam Zuber na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Martin Tiffen akiwa kwenye wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza katika wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akimkabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP) Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Tanzania, Martin Tiffen .
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano pamoja na Menejimenti ya Mradi wa EACOP akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)yaliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………………..
Hafsa Omar-Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amesema kuwa ujenzi wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania( EACOP) unaendelea kutekelezwa kama ulivyopangwa na hautarudi nyuma na tayari nchi zote mbili zipo kwenye hatua za utekelezaji.
Ameyasema hayo, Februari 6,2020 wakati wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Aidha, alieleza kuwa tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kama ulivyopangwa, hatua hizo ni pamoja na kupata eneo ambalo litatumika kuwekea matenki makubwa manne ya mafuta katika kata ya Chongoleani Mkoani Tanga.
Hatua nyingine mbazo Serikali imezichukua ni upatikanaji wa korido ambayo ni njia ya kupitishia bomba yenye kilomita 1414 kwa upande wa Tanzania na kwa ujumla wake zitakuwa 1443 zikijumlishwa na kilomita 300 za upande wa nchi ya Uganda.
Aliongeza kuwa, hatua nyengine ambayo Serikali imechukua ni ukamilishaji wa kufanya kazi ya tathmini ya fidia kwa wale wote ambao watakaopisha eneo la korido hilo ambalo litapita katika wilaya zaidi ya 24 kata 86 na vitongoji 278.
Aliendelea kueleza kuwa, kazi ambazo kwasasa Serikali inazifanya ni pamoja na majadiliaona baina ya nchi mbili husika kuhusu manufaa halisi ya kiuchumi na kijamii katika nchi zote mbili, ambapo ajira zaidi ya 5000 zitapatikana kutokana na mradi huo ajira hizo ni pamoja na ajira za kudumu na ambazo sio za kudumu.
Alisema kuwa, ujenzi wa mradi huo utaanza rasmi mara tu baada ya majadiliano na matayarisho hayo yatakapomalizika na ujenzi wa mradi huo utachukua takribani zaidi ya miezi 36.
Vilevile, amesema jambo hilo la makabidhiano ya cheti cha tathmini lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu na kwasasa limefungua fursa ya kuanza kwenda kwenye hatua ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa na kuwataka wataalamu husika wa mradi kila mtu katika nafasi yake kuanza kutekeleza wa mambo mengine.
Kwa upande wake, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira . Mhe. Mussa Azzan Zungu alisema kuwa hafla hiyo ya kukabidhi Cheti cha Tathmini ya Mazingira kwa Mradi wa EACOP, ni Ushahidi wa Serikali kuridhia kuwa Mradi huu utahakikisha kwamba masuala ya kiuchumi, kijamii,mazingira,afya na usalama yanashughulikiwa wakati wote wa kipindi cha kupanga, kujenga na uendeshaji wa shughuli za bomba ili kupunguza athari kwa mazingira.
Pia,alisema mradi huo wa bomba umezingatia maeneo muhimu ya kimazingira kama vile mbuga za wanyama, Maeneo tengefu kama vile hifadhizi za misitu na maeneo yenye idadi kubwa ya watu.
Aliongeza kusema kuwa, vituo vitawekwa na kuendeshwa kwa umakini ili kupunguza athari yoyote ya kimazingira na kiikolojia wakati wa utekelezaji wa Mradi huu ambao unahitaji ushirikiano baina ya pande tatu Serikali mbili za Tanzania na Uganda pamoja na Wawekezaji.
Aidha, alisema kazi ya Serikali kupitia NEMC haiishii kutoa Cheti tu, bali kuendelea kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake kulingana na masharti ya Cheti kilichotolewa.
“ Timu yangu imejipanga na itaendelea kushirikiana na Wizara ya Nishati ambao ni Msimamizi na Mratibu wa Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania pamoja na wawekezaji pindi watakapoanza kutekeleza Mradi huu kwenye hatua ya ujenzi na uendeshaji ili kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira.”alisema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na Menejimenti ya Mradi wa EACOP.