***************************
Jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewahakikishia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari kwani uhalifu unaendelea kudhibitiwa.
Akizungumza Mkoani humo Kamanda wa polisi wa Mkoa huo SACP- Davide A. Misime amesema kuwa licha ya hali ya usalama kuwa shwari yapo matukio ambayo yamesababisha vifo kwa watanzania wenzetu vilivyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika
mikoa mbalimbali na tukio la waumini waliokuwa kwenye ibada ya maombi kule Mkoani Kilimanjaro kukanyagana na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine takribani 16 kuumia sehemu mbalimbali na
wanaendelea na matibabu.
“Tukio lilitokea Mkoani Kilimanjaro ni tukio baya kwani watanzania wenzetu walikwenda kwenye ibada lakini hawakutarajia wangepoteza maisha. Makongamano na ibada za maombi zimefanywa mara nyingi kupitia
viongozi wa madhehebu mbalimbali na hakuna madhara yaliyotokea”. Amesema SACP- Misime.
Hata hivyo SACP-Misime amesema kuwa Kutokana na hali hiyo ndiyo maana tukio hilo limechukuliwa hadi sasa
kama taarifa ya vifo na siyo mauaji.
“Jeshi la Polisi kama ilivyoelezwa
awali lilimkamata Boniface Mwamposa na wenzake walioandaa kongamano hilo la ibada na kuchukua maelezo yao. Pia uchunguzi wa kina unaendelea kufanywa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na pale ambapo itabainika kwamba kunakosa la jinai lilitendwa na
kupelekea kutokea kwa vifo hivyo na majeruhi hao hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika kwa mujibu wa sheria”. Amesema SACP-Misime