Home Biashara TBL yatoa msaada wa saruji kituo cha afya Iyunga Mbeya

TBL yatoa msaada wa saruji kituo cha afya Iyunga Mbeya

0

Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga,Abdul Kasukari (kushoto),akiongea na ujumbe wa wafanyakazi wa TBL Wakati wa hafla ya kukabidhi masada wa saruji

Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga,Abdul Kasukari (Kulia) akipokea msaada  wa zsaruji kutoka kwa wafanyakazi wa TBL Wakati wa hafla  hiyo

******************************

Katika mwendelezo wa mkakati wake wa kusaidia huduma za kijamii,kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya cha Iyunga kilichopo mkoani Mbeya.

Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa kiwanda cha TBL cha Mbeya,Bw. Godwin Fabian, katika ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Mbeya ambayo inasimamia ujenzi wa kituo hicho.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo,Godwin Fabian, alisema, kampuni ya TBL, itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma katika nyanja mbalimbali hususani za sekta ya elimu,afya,na huduma za maji safi na salama.

“Kupitia  sera ya kampuni ya kuifanya “dunia kuwa maridhawa”kampuni imekuwa mstari wa mbele kusaidia  kukabiliana na changamoto mbalimbali jamii katika jamii kwenye maeneo tunayofanyia biashara zetu”alisema Fabian.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga,Abdul Kasukari, ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa jijini alishukuru kampuni ya TBL, kwa msaada huo  wa kusaidia kufanikisha kituo cha afya cha Iyunga.

“Tunatoa shukrani kwa kampuni yak TBL kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa katika kusaidia jamii, hii inadhihirisha uwekezaji wenu hapa mkoani Mbeya sio wa kibishara tu bali kunufaisha  wananchi wanaoishi mkoani hapa.”alisema Kasukari.