Na.Alex Sonna,Dodoma

Kikundi Cha Kwaya  Ya Bunge kimeaanza Rasmi Kuongoza  Kuimba Wimbo Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki Na Wimbo Wa Taifa Pindi  Shughuli Za Bunge Zinapoanza.

Akizungumza leo , bungeni jijini  Spika  wa  bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai mamlaka aliyonayo  kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia sasa bunge ameliamuru kuwa na desturi ya kuimba nyimbo hizo muhimu pindi  vikao na shughuli za bunge zinapoanza .

Mhe.Ndugai amefafanua kuwa kufanya hivyo itasaidia kwa Watanzania kwa ujumla kuwa na kuwa  na kumbukumbu ya kuzifahamu nyimbo hizo muhimu huku akiwaasa wabunge   wenye vipaji vya uimbaji kujiunga na kwaya hiyo ya Bunge