Home Biashara Changamkieni Fursa! German-Africa Expo & Intern.Afrika Festival Tübingen 2020 Ujerumani

Changamkieni Fursa! German-Africa Expo & Intern.Afrika Festival Tübingen 2020 Ujerumani

0
Watayarishaji wa maonyesho makubwa ya German-Africa International Expo yanaoambata na Afrika International Festival Tübingen,yatakayofanyika kuanzia 27 Julai mpaka 2 Augosti 2020 katika mji wa Tübingen,nchini Ujerumani , wamefungua milango ya maombi kwa wale wanaotaka kushiriki katika maonyesho hayo.
Aidha  kutakuwa na maonyesho ya makampuni ya kiafrika na bidhaa zao,maonyesho ya sanaa na utamaduni,na wale wenye makapuni ya shughuli za utalii wote mnakaribishwa kuwahi fursa ,Pia kutakuwa na semina ya wanahabari ambayo hiyo itakuwa ni maalumu kwa wanahabari wa kiafrika.
Msikose kutumia fursa hii adimu ya kushiriki katika maonyesho haya
ya kimataifa ambayo yana faida kubwa kwa wasanii,wanahabari,wanamitindo na makampuni (SMEs) na bidhaa zenu,nufaika kwa kujitangaza kimataifa.
[email protected], pia unaweza kuwasiliana +255(0)713457743(Shamsa)