Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.Kikao hiki kina lengo la kujadili taarifa za utendaji kazi wa wizara ,bodi za mazao na taasisi zake kwa kipindi cha nusu mwaka kufikia Desemba 2019.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.Kikao hiki kina lengo la kujadili taarifa za utendaji kazi wa wizara ,bodi za mazao na taasisi zake kwa kipindi cha nusu mwaka kufikia Desemba 2019.
******************************
Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula ili watu wake wawe na nguvu ya kufanya kazi kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 Kauli hii ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga leo Jijini Dodoma wakati
akifungua kikao cha nne cha Menejimenti ya wizara kinachojumuisha wakurugenzi,wakuu wa
taasisi na bodi za mazao nchini.
Waziri Hasunga amesema kwa miaka mitatu sasa serikali ya imeendelea kuhakikisha nchi nazalisha mazao mengi na ya kutosha ya chakula kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wizara ya kilimo na taasisi zake.
“Nchi yetu ina utoshelevu wa chakula asilimia 119 mwaka 2019 ambapo tani milioni 16.4 za mazao ya chakula zilizalishwa nchini na zinatumika msimu huu tunapoendelea na msimu wa kilimo ” alisema Waziri wa Kilimo.
Alibainisha kuwa uzalishaji huo wa mazao ya chakula ulishuka ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo nchi ilizalisha tani milioni 16.8 hali inayoifanya nchi kuwa na chakula cha kutosha.
“Kila mtu lazima ale chakula kwa wingi,hivyo jukumu la wizara ya kilimo ni kuhakikisha nchi inazalisha zaidi ili wananchi wawaze kuwa na nguvu za kufanya kazi na kuzalisha malighafi za viwandani” Hasunga.
Amewapongeza wakulima nchini kwa kuitikia wito na maelekezo ya serikali katika kuhakikisha uzalishaji nchini unaendelea kuongezeka hususan kwenye mazao ya chakula na biashara.
Pamoja na utoshelevu huo,waziri wa kilimo amesema kuna mikoa nane (8) yenye halmashauri 44 ina upungufu kidogo wa chakula ambapo serikali tayari imeandaa mpango wa kupeleka chakula toka hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kunusuru hali hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameigiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha inaharakisha upatikanaji na usambazaji wa mbolea aina ya UREA ambayo imeadimika kwa wakulima.
“Wiki za karibuni kumetokea upungufu wa mbolea ya UREA hali inayosababisha kupanda bei na wakulima wengi kulalamika mazao yao kukosa mbolea hii muhimu” Waziri wa kilimo alisema.
Waziri Hasunga ameitaja mikoa ya Ruvuma,Mbeya,Songwe na Njombe kuwa ni maeneo ambayo yana uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula lakini kwa sasa mbolea ya UREA imeadimika.
Ameitaka Menejimementi ya TFRA kuchukua hatua za haraka za usimamizi wa mfumo wa ununuzi mbolea wa pamoja ili wakulima wapate mbolea kwa bei nafuua na kwa wakati .