Home Biashara ASILIMIA 80 YA PAMBA IMESHAUZWA NJE-MHE.BASHE

ASILIMIA 80 YA PAMBA IMESHAUZWA NJE-MHE.BASHE

0

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ,akiongoza kikao na wadau wa tasnia ya  Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao jijini Dodoma kulia kwake ni Mkurugenzi  Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela 

Sehemu ya wadau wa tasnia ya Pamba wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (hayupo pichani) kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ,akizungumza na waandishi wa habari (ghawapo pichani ) mara baada ya kufanya mazungumzo na  wadau wa tasnia ya  Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao jijini Dodoma 

 Mkurugenzi  Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kikao cha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe na  wadau wa tasnia ya  Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao kilichofanyika jijini Dodoma.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe  amefanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya pamba  ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa  kwa msimu ujao.

Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Taasisi za fedha,bodi ya pambaa pamoja na wanunuzi wa pamba  katika kupata mwenendo mzima wa pamba kwa msimu uliopita.

Mhe Bashe  amesema Serikali ilitoa maelekezo katika msimu wa pamba kuwa  pamba yote inunuliwe na sekta binafsi iwapatie fedha kwa ajili ya kununua  na kulikuwa na mapitio kujua hali ikoje na wameuza kiasi gani nje mpaka sasa na kwa takwimu za haraka ni kwamba karibu asilimia 80 imeshauzwa nje  huku msimu mpya umeshaanza .

“ Wakulima safari hii waligaiwa mbegu kwa mkopo wote kwa hiyo tulikuwa tunajaribu kuangalia kwa ajili ya majadiliano ya awali kufanya mapitio ya msimu uliopita vilevile kujiandaa kwa msimu ujao”amesisitiza Mhe.Bashe

Hata hivyo ameongeza kuwa safari hii pamba ilinunuliwa chini ya usimamizi wa serikali  na sekta ya fedha ambapo kulikuwa na makubaliano kati ya serikali na wanunuzi,msimamizi ambaye ni Benki kuu . 

‘’Hivyo kikao hiki ni kwa ajili ya kupitia kwa ufupi, kuangalia  na kupeana muda mpaka wiki ijayo kila mnunuzi alete taarifa ameuza kwa shilingi  ngapi,gharama zake ni shilingi ngapi ili waone ni namna gani ahadi za Serikali zinaenda kwenye utekelezaji’’ Amesema Mhe.Bashe

 Aidha  amesema kuwa jambo jingine muhimu katika majadiliano ni kukubaliana kwamba msimu unaokuja malipo yote yatakuwa kupitiaa benki na  hakutakuwa na mambo yakulipana cash.

“Changamoto ambayo tunayo kwa sasa ni kwamba wanunuzi wanadaiwa fedha za  AMCOS,lakini AMCOS zimetumia fedha za kuwalipa malipo ya wakulima kwa ajili ya kulipia shughuli za uendeshaji  kwa hiyo unakuta kwenye baadhi ya maeneo kuna wakulima wachache wanadai “Ameongeza kusema

 Hata hivyo  Bashe amesema  wanakusanya hizo takwimu kupitia bodi halafu wakishamaliza hii ripoti kupitia kikosi kazi  ambacho kitakuwa kinaongozwa na Mwenyekiti wa Mabenki kwamba kabla ya tarehe 31 januari kuwe tayari na taarifa rasmi .

 Aidha amewaomba  wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya  kutochukua hatua za kutumia nguvu katika kukusanya sec kutoka kwa wafanya biashara kwa sababu kutakuwa na kikao ambacho kitatoa maamuzi ya pamoja  ya malipo ya shilingi 33 kwa ajili ya AMCOS. 

Pia amesema jumla ya kampuni ambazo zimenunua pamba mwaka huu ni 23 kutoka kwa wakulima jumla ya tani 350,000 ambazo zimenunuliwa kiujumla ambazo ni kilo milioni 350 na wafanyabiashara wa Tanzania  wengi wamebaki na kiwango kisichozidi asilimia kumi mpaka sasa.

 Naye Mkurugenzi  Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela   amesema kuwa amefurahishwa na ushirikianao ambao wizara inafanya kati ya taasisi za fedha na wanunuzi wa pamba na kusema kuwa mabenki yalishiriki kwa kina sana  msimu uliopita kwenye kukopesha ambapo wamiliki wa mabenki wameshiriki katika kikao hiki ili kuangalia mwenendo wa ununuzi wa pamba ulivyokwenda.