Home Mchanganyiko TANZIA:MBUNGE WA NEWALA VIJIJINI AFARIKI DUNIA

TANZIA:MBUNGE WA NEWALA VIJIJINI AFARIKI DUNIA

0

Mbunge wa Newala Vijijini, Rashidi Ajali Ahkbar amefariki dunia leo Januari 15, 2020 Mnazi Mmoja mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoani Mtwara, Selemani Sankwa, taarifa za mazishi zitatolewa baada ya makubaliano ya familia na Ofisi za Bunge.

CCM kimesema kinautambua mchango wa kiongozi huo enzi za uhai wake kwa kuwatumikia wananchi wa Newala Vijijini na kujenga chama.