Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akifungua mkutano wa wafanyabiashara wa sekta ya madini kwa ajili ya kutangaza Fursa za kibiashara kwenye sekta ya madini na kuitangaza fursa za sekta hiyo zinazopatikana nchini kwa ujumbe wa Balozi wa China kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru Jijini Arusha
Sehemu ya wafanyabiashara wa sekta ya madini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tamida Sammy Mollel wakimsikiliza Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akifungua mkutano huo wa siku moja kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru jijini Arusha leo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani hapa Zelothe Stephen akihutubia kwenye mkutano wa mabalozi wa Tanzania na China kuelezea fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara wa sekta ya madini mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Hotel ya Mount meru jijini Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa Ofisini kwake na mgeni wake Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke wakizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kwenye Nyanja mbalimbali za kibiashara na maendeleo jijini Arusha
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akibadilisha mazungumzo na Balozi wa China nchini Wang Ke kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kabla ya Balozi huyo kufanya ziara chuo cha Uhasibu Arusha na baadae kwenye mkutano na wafanyabiashara wa sekta ya madini jijini Arusha
Picha na Ahmed Mahmoud Arusha
………………..
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
NAIBU Waziri wa Madini Ladslausi Nyongo amepiga marufuku tabia ya kamatakamata ya wafanyabiashara wa madini nchini waliohifadhi madini maeneo wanayotaka kwa mujibu wa sheria.
Aidha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 Mkoa wa Arusha umekusanya zaidi ya Sh.bilioni 30 zinazotokana na madini ya Vito ya aina mbalimbali.
Akizungumza jana Jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa Mabalozi wa China nchini Tanzania na Tanzania nchini China pamoja na wafanyabiashara wa madini nchini,Naibu Waziri Nyongo alisema sheria inaruhusu wafanyabiashara kukaa na madini ili mradi wafuate sheria.
“Lakini siku za karibuni kumezuka tabia ya kusumbua wafanyabiashara waliofuata sheria za kukaa na madini kwa kulipa kodi zote wanazotakiwa ili wakauze mahali popote wanapotaka,lakini wanasumbuliwa kwa kukamatwa na vyombo vya ulinzi,”alisema.
Alisema ili kuondoa mkanganyiko huo Wizara imejipanga kuelemisha wadau wa madini vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu sheria za madini ikiwemo inayoruhusu wafanyabiashara hao kushikilia madini kabla ya kuuza kwenye soko za madini zilizopo.
Aidha aliomba Mabalozi wa China nchini Tanzania na yule wa Tanzania nchini China kuja kuwekeza nchini kwenye uwekezaji wa uongezaji thamani masini chini ya Gramu mbili ambayo yanaruhusiwa kwenda nje ya nchi bila kuonhezwa thamani.
“Kama mnateknolojia ya kuongeza thamani madini haya tunawaalika mje kuwekeza ili tusiyatoe nje bila kuongeza thamani,”alisema.
Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema wameleta mkutano huo ili kuongeza fursa kwa wafanyabiashara katika kupanua wigo wa soko la madini.
Alisema nchi ya Tanzania ina madini mengi lakini mchango wake kwa pato la Taifa ni asilimia 5.07 tofauti na pato la sekta ya utalii asilimia 17 na asilimia 25 katika kuingizia Taifa fedha za kigeni.
“Mchango huu hautoshi hivyo tumeamua kutumia mkutano huu ili tuongeze fursa katika madini na kukuza zaidi pato la sekta hii,”alisema.
Kuhusu ukusanyaji wa madini alisema yanatokana na soko la madini Namanga kukusanya Sh.bilioni 1.7 ya madini ya vito na soko la Arusha walikusanya Sh.bilioni 34.46 katika kipindi cha Juni 2019 hadi Desemba 2019.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.Idrisa Kikula aliomba Ofisa Madini Mkazi wa Mikoa yote kukaa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuelimishana sheria za madini ili wafahamu jinsi ya kudhibiti utoroshaji wa madini.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliomba wafanyabiashara kutumia fursa ya mkutano huo kuongeza mapato ya madini kutoka Sh.bilioni 500 ya sasa hadi kufikia Sh.Trioni moja.
“China wanunuzi wakubwa wa dhahabu kama mwaka jana 2019 walinunua dhahabu tani 1506 hiki sio kiwango kidogo na hata madini mengine wananunua sana hivyo tujitahidi kuongeza fursa za soko nchini China,”alisema.