Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN ATUNUKU NISHANI ZA MAPINDUZI IKULU ZANZIBAR.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN ATUNUKU NISHANI ZA MAPINDUZI IKULU ZANZIBAR.

0

KATIBU MkuuOfisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Maulid akitowa maelezo ya utowaji wa Nishani za Mapinduzi, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

BAADHI ya Wanafamilia na Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya Utunuku wa Nishani  za Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi wenye Sifaa Maalum, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

BAADHI YA Viongozi wa Serikali wakifuatilia hafla ya Utunuku wa Nishani za Mapinduzi, zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, (kutoka kulia) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, Mhe. Mohammed Faki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, wakifuatilia hafla hiyo.(Picha na IKULU)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza Mfanyabiashara Maarufu Bw. Salim Said Bakhresa baada ya kumtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Wananchi Wenye Sifa Maalum, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za sherhe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wananchi waliotunukiwa Nishani ya Mapinduzi, Nishani ya Utumishi Ulitukuka, na Nishani ya Ushujaa, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)