NA
K-VIS BLOG
NIHATARI
kuegemea au kugusa waya zinazoshikilia nguzo za umeme (Stay wire), Meneja wa
Afya na Usalama Kazini, Shirika la Umeme Nchini Tanesco, Mhandisi Fredy Kayega (pichani) amesema.
Mhandisi
Kayega ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo Desemba 24, 2019 wakati
akizungumzia masuala ya usalama katika miundombinu ya umeme ya Tanesco na hatua
ambazo wananchi wanapaswa kuzingatia ili kuendelea kufaidi huduma ya umeme bila
madhara.
“Napenda
kusisitiza kuwa tunaposafirisha umeme kuna waya tunaita Stay wire, waya huu hutumika kushikilia nguzo, waya huu hutoka juu
ya nguzo mpaka chini ambapo huchimbiwa ardhini, na huwa kuna kifaa kinafungwa
kinachoitwa stay insulator ambapo
huhakikisha kwamba ikitokea kwamba ule waya (Stay wire) kule juu ukigusana na
vile vyuma vyenye umeme kule juu basi umeme usiweze kushuka hadi chini.”
Amefafanua na kuonya………………. ikitokea kuna mvua inanyesha na maji yakatiririka
kupitia ule waya tunatambau kuwa maji husafirisha umeme kwa urahisi na kwakweli
ule waya utakuwa na umeme na mtu anapougusa basi ni wazi kuwa ataathirika moja
kwa moja.” Alisema Mhandisi Kayega.
Alisema
wapo watu hudiriki kuegemea, na wakati mwingine watoto hutumia kubembea hii ni
hatari sana. “Tunaweza kufikiria kuwa waya huu ni waya wa kawaida sana, fikra
hizo si sahihi, waya huo unaweza kuleta madhara wakati wowote, Alionya.
Alisema
kuna watu wamediriki kujenga humba huku waya huo ukiwea ndani, hii ni hatari
waya huu kuna wakati utakuwa na umeme na Ili kuishi vizuri na miundombinu ya
umeme ni vema wananchi tukawa mbali na miundombinu hiyo ili kujiepusha na
madhara yanayoweza kutokea