Home Mchanganyiko WACHIMBAJI MADINI WAOMBA LESENI ZA KANDA

WACHIMBAJI MADINI WAOMBA LESENI ZA KANDA

0
Na.Ashura Mohamed -Arusha.
Wachimbaji,madalali na wafanyabiashara wa  Madini Mkoa wa  Arusha wamemwaomba Waziri Wa Madini Dotto  Biteko leseni za Kanda zitumike nzima ili kuuza Madini ya aina mbalimbali  Kwa Mataifa mengine.
Wameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa Madini  uliohudhuriwa na wafanyabiashara,madalali na wachimbaji pamoja na vyama vya wachimbaji mmoja wa wachimbaji hao Samweli Rugamalira  Amesema nitakribani miaka 8  tangu aanze kazi hiyo ya uchimbaji  Madini aina ya Tanzanite ,ameiomba  wizara kuangalia namna ya kuziboresha na ziweze kutumia  Nchi nzima.
Alieleza changamoto ya ajira ndani ya machimbo ya mererani jambo ambalo  limeibua mjadala kwa wafanyabiashara wanaochimba madini kuwa ni lazima walipie shilingi milioni 400 hadi 500 jambo ambalo limeonekana kuleta utata,  nakumowmba waziri biteko kuingilia kati .
kwa Upande wa madalali  akiwemo Tupilike Samson Mwangosi aliiomba Wizara  kuwatambua na kuwapatia ofisi  ili kuweza kutekeleza kazi zao mana wamekuwa wakifanyabiashara kwa njia ya mali kauli jambo ambalo linafifisha utendaji wao  nakuiomba Tume na wizara kusaidia.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa Madini Tanzania(Tamida) Sammy Mollely alisema wapo tayari kuongeza thamani ya Madini nchini  lakini bado kunachangamoto ya ya vikwazo vya vibali kwa wataalamu wa usanifu,ungarishaji,na uwekaji wa Urembo(nakshi) kuchukuwa muda Mrefu pindi wanapoomba  uku  matarajio yao  nikupata  wataalamu kutoka nchi ya Srilanka ili kuongeza Ujuzi. 
Sammy alisema kuwa uwepo wa  Tasac imekuwa kikwazo kikubwa na kueleza na kero kwao hali inayochangia   kudidimiza uchumi wa nchi,kwani uchukuwa Miezi 2 kupata kibali kusafirisha madini nakueleza ikiwezekana Tasac  Ingeondolewa kwani haina msaada kwao.
Naye Mbunge wa Simanjiro James Olemilya alisema  wilaya hiyo ndiyo  kitovu cha  uchimbaji wa madini lakini  bei ya  Madini  ya Tanzanite imeonekana kuyumba nakuiomba wizara kufanyika uchunguzi wa kina nakubahini kilichojificha ili  kuwabahini watu wanaochezea bei ya Tanzanite na kutokuipatia Nchi  Hasara ..
Waziri wa Madini Mh Dotto Biteko amesema wafanyabiashara wa sekta ya Madini wanayo changamoto yakuifata njia isiyosahihi nakujikuta wanatoka nje ya Mstarikibiashara ,jambo ambalo amesisitiza kufuata hatua zaki sheria kwani sekta hiyo haiwezi kusimamiwa na Waziri mwenyewe uku  serikali ikitaka uwazi wakibiashara na kuhitaji fedha ili kuweza kutekeleza Huduma zakijamii .
Biteko ameongeza kuwa Mheshimwa Rais Wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Maguguli  Anandoto kubwa yakuifikisha Nchi katika Uchumi wakati na anachukizwa na mfanyabiashara anayetorosha Madini na kukwepa kodi ,na kusissitiza  serikali inataka kuvutia wageni kuja kununua Madini kwa haki Nchini.
Naibu Waziri wa Nchi,ofisi ya Waziri mkuu, Sera,bunge kazi, Vijana,na wenye Ulemavu Mh Antony mavunde Amesema nchi inawahitaji wataalamu wa Madini kwa Asilimia kubwa kutoka Nchi ya  Kenya na Srilanka ,nakuanzia  mwakani Wizara yake itaanza kuliwekea mikakati   katika uratibu wa wa vibali vya kazi kwa Wageni ,nakueleza kuwa katika  kutatua changamoto ya vibali Vya kazi   wizara  imekuja na Mfumo mtandao wakupata Kibali cha kazi ili kuondoa urasimu nakupiga marufuku kwa watu wa kati kama waleta maombi, nakuwataka wafanyabiashara kupeleka wenyewe maombi yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe amepongeza utaratibu huo wa Mkoa kukutana na wadau wa Madini  kusikiliza kujadili na  kutatua changamoto zao na kuongeza wigo mpana wakibiashara ndani na nje ya Nchi nakusisitiza  chama kitaendelea kuunga mkono serikali  na kutekeleza ilani ya ccm ikiwemo   wachimbaji kunufaika na sekta hiyo katika   kuongeza  mapato kwani ndiyo dhamira kuu  ya serikali kua  na soko kubwa la  Madini kimataifa duniani.