Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akielekeza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya shule ya msingi
Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Mkoa wa Katavi.
Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda (Tanganyika) kumsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ikiwa ni mwendelezo wa
ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Mkoa wa Katavi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda (Tanganyika) Bi Lilian Matinga akiwasalimu Wananchi, katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
*****************************
Na Rayson Mwaisemba WAMJW- Katavi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani
Katavi ili kupisha uchunguzi.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
“Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika “.Amesema Waziri Ummy.
Aidha,amewataka watumishi wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao.
“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili,weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za nidhamu ikowemo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya
dola”.Amesisitiza Waziri Ummy.