Bw.Dennis Kayanda CEED Balozi akitoa maelezo kwa wajasiriamali umuhimu wa kufuata sheria za kodi
Director wa Shambani Milk na mwanachama wa CEED,Bw.Victor Mfinanga,akitoa soma kwa wajasiriamali jinsi ya kuungana
Director wa Matuli Farm na mwanachama wa CEED,Bw. Jackson,akisisitiza jambo wakati wa semina ya ujasiriamali.
Mwakilishi wa CEED Tanzania,Bw.Fred akieleza kuhusu steji tofauti za biashara
……………….
Kituo cha ujasiriamali cha CEED Tanzania, kimetoa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa wajasiriamali mkoani Morogoro yenye lengo la kuwawezesha namna ya kusimamia biashara zao,kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto za kibiashara pamoja na fursa mbalimbali mkoani humo.
Akizungumza na wajasiriamali wa mkoani Morogoro, Bwana Atiba Amalile, Mkurugenzi wa CEED Tanzania, amewakumbusha wajasiriamali hao kuwa ‘’Haitakuwa biashahara kama kawaida ikiwa Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati miaka ijayo’’.
Naye Bwana Baptist Mnyalape ,mshauri wa masuala ya kodi na mwakilishi wa CEED Tanzania jijini Dodoma amewahimiza wajasiriamali wa morogoro kuhakikisha wanafahamu kanuni zinazoweza kuathiri biashara zao moja kwa moja.
‘’nahitaji kuwakumbusha tu ndugu zangu wajasiriamali kuhusu kuzingatia masuala mazima ya kodi, tuhakikishe tunafahamu kanuni na sheria ambazo zinaweza kuingilia na kuathiri biashara zetu moja kwa moja, ukishindwa kuzingatia haya itagharimu muda wako pamoja na pesa zako. Alisema Bwana Mnyalape.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka CRDB Benki, Bwana Dennis Kayanda amewasisitizia wajasiriamali hao juu ya umuhimu wa kufuata sheria ya matumizi ya ushuru wa ardhi. Akitoa mfano , amesema “ni hatari Zaidi kwa kutafuta mikopo kutoka benki za biashara na kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuwa hazifanyi kazi katika eneo hilo na hivyo kuathiri biashara”.
Naye Bwana Victor Mfinanga mnufaikaji wa mafunzo hayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maziwa Shambani Milk mkoani Morogoro amefurahia kupata nafasi tena kwani mafunzo haya yannamuwezesha kufahamu namna ya kuendesha biashara yake.
‘‘Nimekuwa nikihudhuria mara kwa mara mafunzo ya CEED, mfano mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam na CEED Tanzania yamenisaida kujua habari za biashara bora, namna ambavyo mtu unawezakutumia teknolojia kujifunza namna ya kuendesha biashara yako’’. Alisema Bwana Mfinanga.
Mafunzo hayo yameudhuriwa na wajasiriamali mbalimbali wa mkoani Morogoro, bila kusahau wawakilishi kutoka benki za CRDB, NMB NBC, Azania, pamoja na Benki ya Afrika ambazo kwa pamoja zimewapa elimu wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo bila shida na namna ya kutumia mikopo hiyo kukuza biashara zao.
Vile vile Chama Cha Biashara , Viwanda na Kilimo Tanzania mkoani Morogoro kilipata nafasi ya kushiriki mafunzo haya jinsi ya kukuza na kujenga biashara za ushindani sokoni.